Habari za Punde

Hafla ya uzinduzi wa Zanzibar Startup Association

Katibu Mkuu Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar , Fatma M  Khamis akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Zanzibar Startup Association nd Abdallah Abeid ( kulia) na mtendaji mkuu wa ZSA ndugu Ikram Soraga kushoto
Katibu Mkuu Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar , Fatma M  Khamis akiteta pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Zanzibar Startup Association nd Abdallah Abeid  wakati alipozindua Jumuiya hiyo hapo katika ukumbi wa Sheikh Idris Abdulwakil kikwajuni Unguja.

Katibu Mkuu Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar amezindua Rasmin Jumuiya ya Zanzibar Startup Association iliyoanzishwa kwa lengo la kusimamia na kuwawezesha wajasiriamali Wadogo Wadogo ili waweze kujisimamia katika harakati zao.

Akizungumza mara baada ya Uzinduzi huo Katibu Mkuu ameeleza kuwa jumuiya nyingi huanzishwa lakini kutokana na changamoto mwisho wa siku jumuiya hizo hupotea. hivyo ipo haja ya Jumuiya hiyo kuweka mikakati ya kisera na Sheria zitakazowalinda ili kufikia malengo waliojiwekea . 

Serikali ipo tayari kushirikiana na Startup ili kufanikisha malengo yake “ amesema Katibu . 

Aidha Serikali ipo katika Mpango wa kuanzisha Taasisi Wezeshi kwa lengo la kuwainua wajasiria mali Wadogo wadogo, kwa kuwapatia elimu, Mikopo Na Mitaji itakayowawezesha Na kuwainua wajasiriamali kufika pale wanapopakusudia

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.