Habari za Punde

Warsha ya udhalilishaji wa kijinsia kwa wanafunzi wa skuli za Msingi yafanyika


Na Maulid Yussuf, WEMA
Afisa kutoka kitengo cha Elimu za Elimu za Madrasa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Ukhti Amina Salum Khalfan amesema suala la udhalilishaji lipo tokea enzi za Mitume na hii inaokana na kukosa imani kwa binadamu.

Hayo ameyasema wakati alipofungua warsha juu ya udhalilishaji kwa Wanafunzi wa Skuli ya Msingi Sebleni na Skuli ya Msingi Kilimahewa B, katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari Faraja Unguja.

Amewataka Wanafunzi hao kutokubali kuitwa na watu wasiowajua, kushikwa shikwa wala kupokea zawadi kwani inaweza kuwa ni sababu ya kuanzia vichocheo vya kutaka kudhalilishwa kwa kubakwa na kuwapotezea muelekeo mzima wa masomo yao.
Aidha amewataka Wanafunzi kusoma kwani ni muda wao sasa wa kusoma na kuacha mchezo kwani Elimu ndio msingi mzuri wa maisha yao.
Amewataka Wanafunzi kujitunza kwani masuala ya udhalilishaji yakiwakuta yanaweza kuwapelekea kupata maambukizi ya virusi vya Ukimwi, kupata mimba katika umri mdogo.
Aidha Ukhti Amina amewatahadharisha watoto hao kuacha tabia ya kujidhulumu kwa kujinyonga au kutishia kujiua kwa ajili ya kugombwa na wazazi wao au walimu, kwani kufanya hivyo ni kujiongozea adhabu kubwa kwa mola wao.
Nae Afisa Sheria Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali mwalimu Kondo amesema ipo Sheria ya watoto na hivyo akifanya makosa nae atapelekwa katika mahakama ya watoto na akibainika kosa atahukumiwa.
Aidha amewataka kutoogopa kusema pindi watakapomuona mtu anataka kuwafanyiwa udhalilishaji au wakifanyiwa ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua za Kisheria na kuvitokomeza kabisa vitendo hivyo.
Nao walimu wa Skuli hizo wameushukuru Uongozi wa Wizara ya kwa utaratibu huo walioweka katika kuhakikisha wanawapatia Elimu ya udhalilishaji watoto wao kwani itawasaidia kujiepusha na vitendo hivyo huku wakiwataka wanafunzi hao kuwaelimisha wenzao.
Nao Wanafunzi hao wameiomba Serikali kuongeza adhabu ya kifungo kwa uchache wa miaka sabiini badala ya sitini au kifungo cha maisha kwani imekuwa wamekuwa wakiathirika sana na masuala hayo.
Pia wameoimba Serikali kufungwa CCTV camera katika maeneo yote hatarishi ili kusaidia ushahidi kwa watuhumiwa pamoja na kuhakikisha Sheria zinazotungwa zinafuatwa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.