Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi azindua gati mpya ya Bandari ya Mkokotoni, Unguja

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakipata maelezo ya michoro ya Gati ya Mkokotoni,kutoka kwa Mhandisi wa Wakala wa Majengo Zanzibar (ZBA) Mansour Mohammed,kabla ya kuifungua Gati Mpya ya Bandari ya Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja, ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiondoa kitamba kuweka Jiwe la Msingi la Uzinduzi wa Gati ya Bandari ya Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja,ikiwa ni Shamrashamra za kusherehekea Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar (kushoto kwa Rais) Mkewe Mama Mariam Mwinyi na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja Ndg.Iddi Ame Haji na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Zuberi Ali Maulid.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakipiga makofi baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Ufunguzi wa Gati Mpya ya Bandari ya Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja, ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud,Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “A” Sadifa Juma Khamis,Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja Ndg.Iddi Ame Haji na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Zuberi Ali Maulid(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikata utepe kuashiria kuifungua Gati Mpya ya Bandari ya Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja, ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na (kushoto kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi, Kaimu Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi  Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mhe.Lela Mohammed Mussa na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakitembelea Gati Mpya ya Bandari ya Mkokotoni baada ya kuifungua rasmin leo 4-1-2022, ikiwa ni shamrashamra za Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud.(Picha na Ikulu)
MUONEKANO wa Gati Mpya ya Bandari ya Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja baada ya kufunguliwa rasmin leo 4-1-2022, na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(POicha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akitoa hotuba baada  kuifungua Gati Mpya ya Bandari ya Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja, ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar .(Picha na Ikulu)
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.