Habari za Punde

Rais Mhe Samia atuma salamu za rambirambi kwa Dk Hussein Mwinyi kufuatia ajali ya boti Kisiwa Panza

 Rais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi kufuatia vifo vya watu 10 waliofariki dunia katika ajali boti iliyotokea katika eneo la bahari ya Kisiwa Panza mkoa wa Kusini Pemba.

Rais amemuomba Dkt. Mwinyi kufikisha salamu zake za pole kwa wafiwa wote, ndugu, jamaa pamoja na marafiki na kuongeza kuwa anaungana na familia za marehemu hao katika kipindi hiki cha majonzi.

Watu hao waliofariki dunia walikuwa wanatoka Chakechake kuelekea kwenye mazishi katika Kisiwa Panza.

Rais Samia Suluhu Hassan pia amewaombea kwa Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi, Amina.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.