Habari za Punde

Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe.Zuberi Ali Maulid Ameweka Jiwe la Msingi la Ufunguzi wa Jengo la Hanga la Askari wa KMKM Wete Pemba.

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Zuberi Ali Maulid akiondoka baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Uzinduzi wa Hanga la Asakari wa Kikosi cha KMKM Wete Pemba, ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha sherehe za Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zubeir Ali Maulid amewasisitiza maafisa na wapiganaji wa vikosi vya ulinzi na usalama kuhakikisha wanaendelea kutekeleza majukumu yao kwa nidhamu na uadilifu pamoja na kuyalinda Mapinduzi matukufu ya Zanzibar ili kuweza kudumisha Amani na upendo miongoni mwa Watanzania.

Mhe zubeir ametoa wito huo mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika Hanga la Askari wa KMKM huko Wete ikiwa ni shamra shamra ya kutimiza miaka 58 ya mapinduzi matukufu ya Zanzibar.

Amesema nidhamu na uadilifu katika vikosi vya ulinzi na usalama vitawawezesha  wananchi kushirikiana kwa karibu katika kusimamia Amani na utulivu pamoja na kujiepusha kujiingiza katika makosa mbali mbali ikiwemo magendo na utoaji wa Rushwa hatua inayodhihirisha kuunga mkono dhamira njema ya waasisi wa Taifa.

 

Mapema katibu mkuu wa wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ Issa Mahfoudh Haji na naibu mkuu wa KMKM Kepteni Khatib Khamis  Mwadini wamemueleza Spika Zubeir kwamba mradi huo ni muendelezo wa mpango mkakati wa Serikali wa kumaliza tatizo la makaazi kwa wapiganaji wa kmkm ambapo   Kukamilika kwa jengo hilo kutaleta mapinduzi makubwa katika suala la makaazi kwa wapiganaji wa kmkm hasa wale askari wanaopata uhamisho wa kikazi kutoka unguja kuendelea na kazi kamandi ya pemba.

 

Mradi huo wa ujenzi wa hanga  utaweza kuondoa changamoto ya makaazi kwa wapiganaji wa KMKMK  ambao kwa muda mrefu wamekua wakiishi katika hali ngumu kutokana na uhaba wa nafasi kulinganisha na idadi kubwa ya askari pamoja na uchakavu wa majengo ambayo hayapo salama kwa Maisha ya askari.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.