Habari za Punde

WAZIRI NDALICHAKO AWASILI RASMI OFISI YA WAZIRI MKUU MTUMBA, ASISITIZA USHIRIKIANO

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akisalimiana na Wakuu wa Idara na Vitengo mara baada ya kuwasili katika Ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (kulia) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili rami katika ofisi yake hii leo Januari 10, 2022 katika Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma. Kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Patrobas Katambi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na Wakuu wa Idara na Vitengo walipokuwa wakipokelewa rasmi hii leo Januari 10, 2022 katika Ofisi hiyo Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma.
Sehemu ya Wakuu wa Idara na Vitengo wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (hayupo pichani) wakati wa kikao hicho.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Prof. Jamal Katundu (kushoto) akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako alipowasili katika ofisi hiyo. Kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Patrobas Katambi.

 

PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

Na: Mwandishi Wetu – DODOMA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amewataka watumishi wa ofisi hiyo kushirikiana ili kuleta maendeleo katika Taifa na sekta hiyo ya Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu.

Waziri Ndalichako ameyasema hayo leo Januari 10, 2022 alipokuwa akizungumza na watumishi wa ofisi hiyo mara baada ya viongozi kuteuliwa kuongoza Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan hivi karibuni wakiwemo na Naibu Waziri Mhe. Patrobas Katambi pamoja na Katibu Mkuu, Prof. Jamal Katundu.

“Namshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuniamini na kutupa nafasi mimi pamoja na Naibu Waziri na Katibu Mkuu ya kuwepo katika Ofisi hii ya Waziri Mkuu,” alieleza

“Niwaombe watumishi kuimarisha ushirikiano ili maeneo haya yote manne yaani Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu yatekelezwe ipasavyo,” alisema Waziri. Prof. Ndalichako

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.