Habari za Punde

ACT – Wazalendo kimewataka wanachama wake kurudi kuungana na viongozi waliochaguliwa ili kufanikisha malengo waliyojiwekea.

 

Makamu Mwenyekiti Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, walipowasalimia  wanachama katika ufunguzi wa Tawi jipya la Chama hicho huko Kangagani, jimbo la Kojani Mkoa wa Kaskazini Pemba, lilopewa jina la 'Nelson Chamisa' ambaye ni Rais wa chama cha Upinzani cha (CCC) nchini Zimbabwe.

Kauli hio imetolewa jana  na viongozi Wakuu wa Chama hicho  wakiwemo Kiongozi wa Chama Zito Zuber Kabwe, Mwenyekiti wa Chama Ndugu Juma Duni Haji pamoja na Makamu Mwenyekiti Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, walipowasalimia  wanachama katika ufunguzi wa Tawi jipya la Chama hicho huko Kangagani, jimbo la Kojani Mkoa wa Kaskazini Pemba, lilopewa jina la 'Nelson Chamisa' ambaye ni Rais wa chama cha Upinzani cha (CCC) nchini Zimbabwe .

Wamewataka wanachama walioanza kuyumba kimawazo kutokana na kukosa kuteuliwa katika nafasi mbali mbali za uteuzi  wasijiondoe na badala yake warudi na  kuungana na viongozi wapya ili kuendeleza juhudi za marehemu Maalim Seif za kupigania haki, usawa na Demokrasia Zanzibar.

Viongozi hao wameeleza kwamba uchaguzi wa chama hicho uliendeshwa kwa misingi ya Kidemokrasia, haki na kupewa Baraka na  mamlaka na taasisi mbali mbali na kwamba kinachohitajika sasa ni kushikamana ili kutetea maendeleo kwa maslahi ya jamii umma na Tanzania kwa ujumla.

Makamu Mwenyekiti wa ACT- Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, amewataka wanachama hao kurudi kwenye chama chao na watapokelewa kuendeleza juhudi za kukijenga na kutekeleza dhamira ya Maalim seif ya kuitetea Zanzibar.

"Milango ipo wazo hivyo wanachama wenzangu ni vyema mukarudi  katika chama chenu ili tuendelee kuunga mkono chama ambacho kina malengo makubwa na ni chama cha wote", alisema Mhe. Othman ambae pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.

Naye Kiongozi wa Chama ndugu Zito Zuberi Kabwe amewaeleza wananchama hao kwamba ni busara kuthamini juhuidi zilizoasisiwa na Maalim Seif na kwamba chama hicho ndicho kilichopewa baraka na kiongozi huyo ambaye ametangulia mbele ya haki.

Amesema sio busara watu kupoteza mwelekeo wakasahau juhudi za kiongozi huyo ambaye ametumia uhai wake wote  kuyapigania maslahi na heshima ya visiwa vya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

Naye Mwenyekiti wa Chama hicho Babu Juma Duni Haji, amewakumbusha wananchi kwamba  viongozi wa ACT Wazalendo kamwe sio wa uchu na tamaa ya madaraka, na badala yake wanapigania haki ya wanyonge na zaidi kizazi cha wazanzibari ambacho kimeachwa muda mrefu bila matumaini.

“Sisi tumenyanyaswa, tumepigwa, tumefungwa na kufanyiwa kila aina ya visingizio, lakini hatukati tama kwa kuwa lengo letu ni hawa", alisema Babu Duni huku akiashiria mtoto wa miaka 9 aliyempandisha jukwaani kutoa vilelezo vya ithibati ya hali mbaya ya maisha ya watu iliyopo hivi sasa.

Tawi hilo jipya la Chamisa lilolofunguliwa jana februari 13,limesajili zaidi ya wanachama wapya 168 kwa njia ya ACT- Kiganjani ambapo wanachama 20 walikabidhiwa kadi katika hafla hiyo kwa niaba yawengine na usajili unaendelea  kuwapata wanachama wapya zaidi tawini hapo.

Kitengo cha Habari 
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
14/02/2022.






No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.