Habari za Punde

Rais wa Zanzibar Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Ametuma Salamu za Rambirambi kwa Mzee Malecela.

 


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya Mzee John Malecela kufuatia kifo cha mpendwa wao Mwelentuli Malecela.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi ametoa salamu hizo za pole kwa ndugu jamaa na marafiki pamoja na uongozi wote wa Shirika la Afya Duniani (WHO), ambapo marehemu  hadi umauti unamfika alikuwa ni Mkurugenzi  wa Udhibiti wa Magonjwa yasiyopewa Kipaumbele.

Katika salamu hizo za rambirambi, Rais Dk. Mwinyi alieleza kusikitishwa na kifo hicho na kuwanasihi ndugu, jamaa na marafiki pamoja na uongozi wote wa (WHO) kuwa na subira na ustahamilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo.

Rais Dk. Mwinyi amemuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu mahala pema peponi,  Amin.

Marehemu Mwelentuli alizaliwa Machi 26, 1963  ambapo katika uhai wake aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Tafiti za kiafya Tanzania (NIMRI) ambapo pia, aliwahi kuwania nafasi ya mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Imetayarishwa na Kitengo cha Habari,

Ikulu Zanzibar.AL OF RESPONSIBILITY!RS ABUSE@THEWORLDNE

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.