Habari za Punde

TPA Tanga Watumia Maonesho ya TANZFOOD EXPO 2022 Jijini Arusha Kujitangaza.

Afisa Uhusiano wa TPA Tanga Adam Mshindo akizungumza na wafanyabiashara waliotembelea banda lao wakati wa maonyesho makubwa ya Kilimo na Chakula maarufu kama (TANZ FOOD EXPO 2022yaliyofanyika Jijiji Arusha

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari ya Tanzania Tawi la Tanga wameshiriki maonyesho makubwa ya Kilimo na Chakula maarufu kama (TANZ FOOD EXPO 2022 huku wakiwataka wafanyabiashara kutoka mkoa ya Kanda ya Kaskazini kutumia Bandari ya Tanga kutokana na maboresho makubwa yaliyofanywa na Serikali.

Akizungumza wakati wa maonyesho hayo ambayo wametumia kama njia ya kutangaza fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye Bandari hiyo ,Afisa Uhusiano wa TPA Tanga Adam Mshindo alisema Serikali imefanya maboresha makubwa ambayo yataongeza ufanisi mkubwa katika Bandari hiyo.

Alisema pia wamekwenda kushiriki maonyesho hayo kutokana na kwamba wao ni wadau wake wanashiriki kwenye maonyesho hayo wanatumia bandari ya Tanga kusafirisha mizigo yao na kujitangaza.

Awali akizungumza wakati wa maonyesho hayo Mhandisi kutoka Bandari ya Tanga Hamisi Kipalu alisema kwa sasa wanaendelea na mradi mkubwa wa uboreshaji wa Bandari ya Tanga kwa awamu ya pili mradi wa ujenzi wa gati namba moja na namba mbili wenye urefu wa mita 450.

Alisema ujenzi huo unatekelezwa na mkandarasi kutoka nchini China akisimamiwa na mwandisi Mshauri Kampuni ya NIRAS kutoka nchini Denmark akishirikiana na Kampuni ya Kitanzania NovakKauli hiyo iliungwa mkono pia na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Ms Regine Hess ambaye naye aliupongeza mchango wa bandari katika kuendeleza shughuli mbalimbali ikiwemo za kilimo

Alisema faida za mradi huo ni kubwa kutokana na kwamba itasaidia kuongeza ufanisi wa bandari hiyo sambamba na kufungua biashara na kuongeza wateja kwenye ukanda wa Afrika Mashariki.

Maonyesho hayo yalifunguliwa na Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela ambae aliupongeza mchango wa Bandari katika kuendeleza kilimo na kufikisha mazao katika masoko ya kitaifa na kimataifa.

RC Mongela alisema maonyesho hayo ambayo yalifanyika kwa siku tatu kwenye viwanja vya Magereza Kisongo mkoani humo yalitoa fursa atengea muda waje kupata elimu ya bure na inafaida kubwa sana

Hata hivyo Mratibu wa Maonyesho hayo Dominiki Shoo alisema maonyesho hayo yatakuwa yanafayika kila mwaka na lengo kufungua milango kwa wakulima.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.