Habari za Punde

Viwanda vikubwa vya uwekezaji kujengwa nchini

Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Omar Said  Shaaban akizungumza katika kikao maalum cha kujadili fursa za uwekezaji katika vipau mbele vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikiwemo viwanda, uchumi wa buluu,Miundombinu na Teknolojia ,majadiliano hayo yalikua  kati ya Mawaziri wa Wizara zilizopewa vipau mbele na Wawekezaji kutoka Nchi ya Quweit na Uturuki huko Ukumbi wa Zura Maisara Zanzibar.

PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR.

NA RAHMA KHAMIS MAELEZO ZANZIBAR                                          11 .03.2022

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar   kupitia Wizara ya  Biashara na Maendeleo ya Viwanda  imesema inakusudia  kujenga Viwanda Vikubwa vya uwekezaji ili kuwainua Wananchi Kiuchumi

Akizungumza  katika kikao maalum Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Omar Said  Shaaban   huko katika Ukumbi wa Zura Maisara na  wawekezaji kutoka Nchi ya Kuwait na Uturuki amesema ujio wao ni ishara tosha ya kuonyesha utayari wao katika kuisaidia Zanzibar Kiuchumi.

Amesema Serikali imetoa vipao mbele kwa baadhi ya maeneo ikiwemo Uchumi wa Buluu,miundombinu, Nishati pamoja Viwanda  ili kuwawezesha wananchi kujiinua kiuchumi na kuleta maendeleo katika Nchi .

Amesema ujio wa wawekezaji Nchini utasaidia kuimarisha huduma muhimu ambazo zikikosekana itapelekea Nchi kuwa Nyuma Kimaendeleo na kusababisha ukosefu wa ajira kwa wananchi.

 Aidha amefahamisha kuwa wawekezaji hao watawekeza katika maeneo yaliopewa kipaumbele na Serikali ikiwemo Viwanda vya Usalama wa Chakula na Viwanda vya  Nishati ikiwa ni mahitaji muhimu kwa wananchi na kulifanya Taifa Kuweza kujitegemea hasa wakati wa Majanga.

Nao wawekezaji hao wamesema  wapo tayari kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwekeza hasa maeneo yaliyopewa  vipao mbele na  serikali ili kuliongezea pato la Taifa.

Kikao hicho kimewashirikisha watendaji wa (SMZ)ikiwemo Mawaziri,Manaibu Waziri na Makatibu Wakuu wa Wizara zilizopewa vipaumbele na kujadili mambo mbalimbali ya kimaendeleo nchini.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.