Habari za Punde

DC Moyo Amewataka UVCCM Mkoani Iringa Kuulinda Muungano wa Tanzania.

Mkuu wa Wilaya ambae ni Kamisaa wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Iringa (CCM) Mhe.Mohamed Hassan Moyo akizungumza na baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi waliokuwa wamejitokeza kwenye kongamano maalum la UVCCM Mkoa wa Iringa
Baadhi ya wanachama wa chama cha mapinduzi waliokuwa wamejitokeza kwenye kongamano maalum la UVCCM mkoa wa Iringa

Na Fredy Mgunda,Iringa.

Mkuu wa wilaya ambaye ni kamisaa wa chama cha mapinduzi wilaya ya Iringa (CCM) Mohamed Hassan Moyo aliwataka vijana wa chama cha mapinduzi kuendelea kuelezea mafanikio ya muungano wa Tanzania kwa namna ambavyo serikali kwa kipindi chote ilivyofanya kazi kuleta maendeleo.


Akizungumza kwenye kongamano maalumu la umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi mkoa wa iringa (UVCCM),Moyo alisema kuwa kumeibuka wimbi la watu ambao wanataka kuuvunja muungano kwa maslai yao.


Alisema wapo watu hawataki kuona muungano huo ukiendelea kuimarika hivyo jumuiya ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi wanapaswa kuendelea kuulinda muungano ili usivunjike.


Moyo alisema kuwa vijana wanawajibu wa kuwapinga watu wote ambao wanampango wa kuuvunja muungano kwa nia ovu zao hivyo vijana ndio wanajukumu la kuulinda muungano.


Aidha Moyo aliwataka vijana wa chama hicho wanaoenda kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwenda kushiriki uchaguzi kwa uadilifu ili kupata viongozi walio imara na bora kukiongoza chama hicho.


Alisema kuwa vijana wanaoenda kugombea wanatakiwa kuwa wanaccm kweli na sio mamluki wanaopandikizwa kwa lengo la kuja kukivuruga chama hicho hivyo wanatakiwa kuwa makini kwenye chaguzi za chama.

Moyo alisema kuwa uongozi wa serikali ya wilaya ya Iringa hautakubari kuona wagombea wanashinda kwa kutoa rushwa hivyo TAKUKURU itakuwa macho muda wote.


Alisema lengo la uchaguzi huo ni kupata viongozi safi ambao watakiongoza chama hicho kwa mafanikio ya kukivusha chama hicho kwenye chaguzi mbalimbali ambazo chama hicho kitashiriki kutafuta mamlaka ya kuunda serikali.


kwa upande wake katibu mkuu wa umoja wa Vijana
(UVCCM) taifa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo,Kenani Kihongosi alisema kuwa katiba ya chama cha mapinduzi inamtaka mwanachama yeyote anahaki ya kugombea nafasi yoyote bila ya kuwa na uwoga wowote ule.


Kihongosi aliwata vijana wa UVCCM kuacha tabia ya kulalamika kuwa wananyimwa nafasi za uongozi lakini kipindi cha uchaguzi vijana hao hawajitokezi kugombea.

Kihongosi alisema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anawaamini vijana ndio maana kwenye teuzi mbalimbali za serikali,ameteua Zaidi ya asilimia 75 hadi themanini za vijana kwenye kuongoza serikali ya awamu ya sita.


Aliagiza kwa makatibu wote wa UVCCM Tanzania kuacha mara moja kuwabeba wagombea,waache wanachama waamue nani anastahili kuwa kiongozi wa chama hicho ambaye anauwezo wa kuongoza jumuiya hiyo na chama kwa ujumla.


Kihongosi alisema kuwa hataki kusikia fomu za wagombea zinapotelea ofisini bali fomu zote zinatakiwa kufika sehemu husika ili vikao husika viweze kutoa maamuzi kwa mjibu wa katiba ya chama.


Alisema kuwa katika uchaguzi wa mwaka huu atasimamia kanuni na sheria za chama hicho ili kupata viongozi bora ambao wataweza kukiongoza chama hicho na wanachama chake kwa kuwa rushwa haina nafasi mwaka huu.

Aidha Kihongosi aliwataka vijana wa umoja huo kucha tabia ya kuwapiga majungu vijana wenzao ili kila mmoja apate nafasi anayostahili kulingana na nafasi anayoishika naanayoigombea.

“Ni marufuku kwa viongozi kupanga safu katika uchaguzi wa mwaka huu kwa kuwa kufanya hivyo kutapekea chama kupata viongozi wabovu ambao hawastahili kuwa viongozi” alisema Kihongosi


Kihongosi amewataka vijana wa umoja huo kwenda kugombea nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi wa chama kulingana na uwezo wako.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.