Habari za Punde

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan afunga Mkutano Maalum wa CCM Taifa Jijini Dodoma

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo wakati akiondoka katika ukumbi wa Jakaya Kikwete mara baada ya kufunga Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo kutoka kwa Wazee nchini kwa kutambua na kuthamini mchango wake mkubwa wa kuleta maendeleo nchini kabla ya kufunga Mkutano Mkuu Maalum wa CCM uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 01 Aprili, 2022.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali, Wanachama pamoja na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa wakati akifunga Mkutano huo Maalum uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 01 Aprili, 2022.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa chama na serikali wakiwa pamoja na wastaafu

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.