Habari za Punde

Viongozi wa Baraza la wafanyakazi la sekretarieti ya Mkoa wa Morogoro kuwashirikisha wafanyakazi katika Idara, vitengo na Taasisi zao

Na.Andrew Charles.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela amewataka viongozi wa Baraza la wafanyakazi la sekretarieti ya Mkoa wa Morogoro kuwashirikisha wafanyakazi katika Idara, vitengo na Taasisi zao ili kuwasaidia kufanya tathimni na kutanua wigo katika kufanya maamuzi.

Shigela ameyasema hayo April 21 mwaka huu katika kikao cha Baraza hilo kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwaa jili ya kuunda baraza jipya la wafanya kazi baada ya baraza lililokuwepo awali kumaliza muda wake.

Mkuu huyo wa Mkoa ameeleza kuwa kuna mambo ya msingi ambayo viongozi hao wanatakiwa kujipanga vizuri kuyatekeleza kwa wakati ili yaweze kuleta tija katika maendeleo ya wananchi.

Yako mambo ya msingi yanayohitaji mabadiliko ya maendeleo kwa  wananchi wa Mkoa wa Morogoro kwa hiyo ni lazima kama wafanyakazi tukajiangalia nafasi yetu hiyo sio nafasi ya kutoka nyumbani kuja Ofisini, nachangia nini katika transformation ya Mkoa wa Morogoro katika maendeleo Martine Shigela amesema.  

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa amewataka wajumbe wa Baraza hilo kutumia fursa ya nafasi zao hizo kutathmini ni upi mchango wao katika kuhakikisha wanaboresha maendeleo ya wananchi wa Morogoro na watanzania kwa jumla na badala ya kuangalia wananufaikaje wao binafsi.

Mwenyekiti Mpya wa Baraza hilo Erick Olomi ambaye ni Mchumi kutoka Idara ya Mipango na Uratibu Ofisi ya Mkuu wa Mkoa amesema Baraza hilo limenzishwa kwa lengo la kuwaunganisha na kuwashirikisha wafanyakazi kutoa maamuzi katika Idara zao huku akiahidi kuboresha maeneo muhimu ikiwemo kipengele cha kusimamia sheria mbalimbali na miiko ya kazi.

Kwa upande wake Oltelmas Tarimo ambaye ni Katibu wa chama cha wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) Mkoa wa Morogoro amebainisha kuwa pamoja na mambo mengine Baraza hilo linawajibu wa kupitia bajeti za taasisi ili wafanyakazi waweze kujua maslahi yao na haki wanazotakiwa kuzipata.

Wanawajibu wa kujua ni nini ambacho kimetengwa kwenye bajeti kwa hiyo tunapokuwa na baraza la wafanyakazi linawasaidia kwanza wafanyakazi kujua ni nini ambacho kimepangwa kwenye bajeti kwa maana ya kwamba mishahara, miradi ya maendeleo, na mipango kazi ambayo ipo na kimsingi wanakuwa wanajua maslahi yao ambayo yamekuwa yameandaliwa kwa mwaka husika Ameeleza Tarimo.

Miongoni mwa Wajumbe wa Baraza hilo Yohana Kasetila ambaye ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilosa ameeleza umuhim wa mabaraza hayo kuwa yamekuwa msaada mkubwa katika kutatua migogoro mahala pa kazi kutokana na uwazi na ushirikishwaji wa Wafanyakazi wa ngazi ya chini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.