Habari za Punde

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akutana na Kuzungumza na Viongozi Wakuu wa CHADEMA Ikulu Chamwino Jijini Dodoma

Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Abdulrahman Kinana akizungumza na Katibu Mkuu wa Chama hicho Daniel Chongolo katika Kikao cha pamoja na Wajumbe wa CHADEMA, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza Kikao cha majadiliano pamoja na Viongozi Wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Ikulu Chamwino Jijini Dodoma tarehe 20 Mei, 2022. Baadhi ya Viongozi wa CHADEMA waliohudhuria Kikao hicho ni Mwenyekiti Freeman Mbowe, Makamu Mwenyekiti Zanzibar Saidi Issa Mohamed, Katibu Mkuu wa Chama hicho John Mnyika pamoja na Baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu na Sekretarieti ya Chama hicho.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar, Saidi Issa Mohamed na Baadhi ya Wajumbe wengine wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Baadhi ya Viongozi wa CCM pamoja na Serikali Ikulu Chamwino tarehe 20 Mei, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Abdulrahman Kinana mara baada ya Kikao kilichofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei, 2022.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.