Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Amekutana na Kuzungumza na Ujumbe wa Taasisi ya Munadhamat Al Dawa Al Islamia Ikulu leo 24-5-2022.

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Ujumbe wa Taasisi ya Munadhamat Al Dawa Al Islamia ukiongozwa na Mwenyekiti wake  Sheikh Abdulrahaman Abdulla (kulia kwa Rais) walipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha mazungumzo yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu leo 24-5-2022.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mwenyekiti wa Taasisi ya Munadhamat Al Dawa Al Islamia Sheikh.Abdulrahaman Abdulla, (kulia kwa Rais) na Katibu Mkuu wa Taasisi hiyo  Bw.Attah Mannan Bakhit walipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha, mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar leo 24-5-2022, akiwa na Ujumbe wake
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuagana na Ujumbe wa Taasisi ya Munadhamat Al Dawa Al Islamia ukiongozwa na Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Sheikh.Abdulrahaman Abdulla.(mwenye kilemba) baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 24-5-2022
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na mgeni wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Munadhamat Al Dawa Al Islamia Sheikh.Abdulrahaman Abdulla, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 24-5-2022.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi   Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali inathamini na kuunga mkono misaada mbali mbali inayotolewa na  Jumuiya zisizo za Kiserikali katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar.

Dk. Mwinyi amesema hayo leo wakati alipokuwa na mazungumzo na Masheikh kutoka Jumuiya ya Munadhamat Al Dawa Al Islamia, Ikulu Jijini Zanzibar, ikiwa ni hatua ya kuendeleza mashirikiano kati ya Jumuiya hiyo na Zanzibar.

Alisema Serikali inathamini juhudi mbali mbali zinazofanywa na Jumuiya zisizo za Kiserikali katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar,  kwa kuzingatia kuwa haina uwezo wa kukidhi mahitaji yote ya kijamii kwa wananchi wake..

Alisema juhudi zinazofanywa na Jumuiya hiyo katika uimarishaji wa  huduma mbali mbali za kijamii; ikiwemo elimu, afya, maji safi na salama, makazi kwa watoto wa mitaani, huduma kwa mayatima pamoja na wajane,  ni miongoni mwa vipaumbele vya Serikali, hivyo akapongeza mashirikiano yaliopo kati yake na Serikali yenye lengo la kuwaondolewa changamoto wananchi.

Aidha, Dk. Mwinyi alionyesha furaha yake kwa viongozi wa Jumuiya hiyo kwa kufanya kazi pamoja na Serikali na kusema Serikali itaendeleza mashirkiano hayo ili kuzitafutia ufumbuzi changamoto zote zitakazojitokeza katika utekelezaji wa miradi mbali mbali.

Sambamba na hayo, aliipongeza Jumuiya hiyo kwa kufanya kazi kwa weledi na uwazi pamoja na mashirkiano yake katika kusaidia sekta ya elimu ya juu nchini kupitia Chuo Kikuu cha Zanzibar (ZU).

Alieleza  elimu ni muhimu katika kuleta mageuzi ya kiuchumi,hivyo akasisitiza umuhimu wa vijana kupata elimu katika Vyuo vikuu pamoja na Vyuo vya Ufundi ili hatimae waweze kujenga uwezo wa kufanyakazi.

Nae, Kiongozi wa Jumuiya hiyo Sheikh Abdulrahman Abdulla kutoka nchini Qatar alisema Jumuiya hiyo imekuwa na ushirikiano na uhusiano wa Kihistoria kati yake na Tanzania pamoja na Zanzibar, na kutekeleza miradi mbali mbali ya kijamii, hususan katika sekta za Elimu ya Juu pamoja na Afya.

Alise jumuiya hiyo itafanya kila linalowezekana kuisaidia Zanzibar kupitia sekta hizo za Kijamii.

Jumuiya ya Munadhamat Al Dawa Al Islamia, ambapo ina Tawi lake nchini Tanzania inajishughulisha na utekelezaji wa miradi tofauti ya Kijamii katika nchi mbali mbali za kiafrika.

Imetayarishwa na Idaya ya Mawasiliano

Ikulu Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.