Habari za Punde

DC MOYO AWAPIGA MAGOTI WAZEE WA KIMILA WARUHUSU MAJI YAFIKE KWENYE UJENZI WA SHULE YA MLENGE

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe.Mohamed Hassan Moyo akiwaonyesha Wamzee namna gani ambavyo Mradi wa Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Mlenge ulivyokwama kutoka na maji kutofika eneo la mradi kwa kusadikika kuwepo Imani za kishirikina.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe.Mohamed Hassan Moyo akiwa kwenye picha ya pamoja na wazee wa kimila wa Kijiji cha Mlenge tarafa ya Pawaga wakijadiliana namna ya kutatua changamoto ya maji kutofika eneo la mradi wa ujenzi wa shule ya sekondari ya Mlenge
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiwa kwenye picha ya pamoja na wazee wa kimila wa Kijiji cha Mlenge tarafa ya Pawaga wakijadiliana namna ya kutatua changamoto ya maji kutofika eneo la mradi wa ujenzi wa shule ya sekondari ya Mlenge.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiwa kwenye picha ya pamoja na wazee wa kimila wa Kijiji cha Mlenge tarafa ya Pawaga wakijadiliana namna ya kutatua changamoto ya maji kutofika eneo la mradi wa ujenzi wa shule ya sekondari ya Mlenge

Na Fredy Mgunda, Iringa.

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo amelazimika kuwaomba wazee wa Kijiji cha Mlenge kufanya tambiko maalum ili kutatua hali ya sintofamu ya bomba la maji kushindwa kufikisha maji katika eneo la mradi wa ujenzi wa Shule

Inaelezwa kuwa uenda miongoni mwa wazee wamechukizwa na upitishwaji wa bomba hilo katika mashamba yao pasipo kushirikishwa hivyo wameyazuia kimiujiza maji hayo kufika eneo la mradi mpaka pale watakapoombwa radhi

Hata hivyo kwa mujibu wa kikao maalum baina ya Mkuu wa Wilaya na Wazee hao makubaliano yaliyofikiwa ni kufanyika tambiko ambapo mkuu Tambiko amemhakikishia mkuu wa wilaya kuwa maji hayo yataanza kutoka

Akizungumza na wazee hao mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa haiwezekani maji yananguvu kubwa ya kufika kwenye eneo la mradi lakini yanaishia njiani Jambo ambalo sio sawa.

Moyo alisema kuwa kama Kuna mzee au mwananchi anamanung'uniko kuhusu mradi huo aseme ili waweze kutatua changamoto hiyo na mradi uendelee kujengwa kwa kuwa muda sio rafiki.

Alisema kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan imeleta fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule hivyo ujenzi usipofanyika kwa wakati fedha zote zitarudi serikalini na mradi huo watakuwa wameukosa.

Moyo aliwaomba wazee wa Kijiji na wazee wa mila kufanya jambo ambalo litasaidia kuendelea kwa mradi wa ujenzi wa shule ya sekondari ya Mlenge iliyopo tarafa ya Pawaga.

Kwa upande wao wananchi na wazee wa Kijiji cha Mlenge walisema kuwa watakaa kikao maalumu cha kushughulikia kero hiyo na kumuahidi mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo kuwa watatau tatizo hilo mapema iwezekavyo tena mara baada ya kikao.

Walisema kuwa ni kweli kuna baadhi ya wazee wanamanung'uniko kutokana na kutoahirikishwa kwenye mradi huo wa ujenzi wa shule ya sekondari Mlenge na hata eneo ambalo wamepitisha bomba la maji ni shamba la mtu ambaye alikuwa bado hajavuna mazao yake.

Walisema kuwa wapo tayari kukaa na wenzao na kufanya tambiko ambalo litasaidia kuendelea kwa mradi huo wa ujenzi wa shule ya sekondari Mlenge ambayo itawapunguzia Wanafunzi kusafiri umbali mrefu kufuata huduma ya elimu.

Wazee hao walimalizia kwa kusema kuwa Serikali inapochukua maeneo ya wananchi wanapaswa kutoa taarifa mapema na kuwashirikisha ili kusitokee changamoto kama ambazo zimetokea.

Naye mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Bashir Muhoja alisema kuwa wamejipanga kuhakikisha mradi huo unaendelea kwa kupeleka gari la kuchotea maji kutoka mtoni na kupeleka eneo la mradi huo wa ujenzi wa shule ya sekondari Mlenge.

Muhoja alisema kuwa wameongea na fundi anayetengeneza tofari kuwa ahamie eneo lenye maji na aanze kufyatua tofali hizo mara moja ili mradi uendane na kasi ya muda unaotakiwa mradi kukamilika.

Alimazia kwa kuwaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali kwenye miradi mbalimbali ya kimaendeleo. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.