Habari za Punde

Mageuzi ya Elimu Yazingatie Mipango Makini.

 

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman,akiwasalimia na kuwafariji wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya ufundi Kengeja iliyopo Mkoa wa Kusini Pemba, kufuatia tukio la  kuungua moto kwa mabweni ya wasichana katikati ya Mwezi wa Mei, mwaka huu ikiwa ni katika ziara yake ya kutambua changamoto zinazoikabili sekta ya Elimu Zanzibar kwalengo la kuitafutia ufumbuzi,
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman,akifuatilia kwa makini somo la vitendo kutoka kwa wanafunzi wa kidato cha nne wa Skuli ya Pindua Sekondari ya kusini Pemba, wakiongozwa na Kijana Abubakar Said Bakar akitoa ufafanuzi namna ya kutambua udongo salama na usiosalama kwa kilimo, katika ziara yake ya kutambua changamoto zinazoikabili sekta ya Elimu Zanzibar kwalengo la kuitafutia utatuzi,
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman,akizungumza na viongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, wakandarasi na wananchi mbalimbali mara baada ya kukagua ujenzi wa skuli ya Elimu Mjumuisho iliyopo Pujini Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba katika ziara yake ya kutambua changamoto zinazoikabili sekta ya Elimu Zanzibar kwalengo la kuitafutia ufumbuzi,

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman, amesema Serikali itahakikisha inaandaa mipango bora ya kukuza Sekta ya Elimu ili kwenda sambamba na mabadiliko ya sasa ulimwenguni yanayotegemea sana taaluma za ufundi, sayansi na teknolojia.

Mheshimiwa Othman ameyasema hayo Juni 1,2022 kisiwani Pemba katika ziara yake maalum ya kikazi ambayo imejumuisha pia ukaguzi wa miradi mbalimbali ya kuendeleza sekta ya elimu hapa Visiwani.

Amesema kuwa ni wajibu wa Serikali kwa sasa kuwekeza katika kufanikisha elimu itakayotoa wasomi bora wa kada tofauti zikiwemo za ufundi, ambapo hilo litawezekana kwa mamlaka zinazosimamia sekta hiyo kuandaa mipango makini.

Mhe. Othman ambaye katika ziara hiyo ameambatana na Mke wake, Mama Zainab Kombo Shaib, alikagua Ujenzi wa Madarasa Matano katika Skuli ya Mizingani, kukagua maendeleo ya Skuli ya Pindua, Kituo cha Elimu Mjumuisho cha Pujini na Skuli ya Sekondari ya Madungu, zote katika Mkoa wa Kusini Pemba.

Kabla ya hapo Mhe. Othman alipita kusalimia, kuwafariji wahusika na kutembelea Mabweni ya Skuli ya Ufundi ya Kengeja, ambayo yaliteketea vibaya kwa kuungua moto, katikati ya Mwezi wa Mei, 2022.

Kufuatia tukio hilo Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Bw. Mattar Zahor Masoud, aliiarifu hadhira hiyo kwamba tayari ameshapokea Ripoti ya Uchunguzi kupitia Kamati aliyoiunda mara tu baada ya ajali hiyo.

Ziara hiyo imewajumuisha Viongozi mbali mbali wa Serikali, Jamii, Vikosi vya Ulinzi na Usalama, Vyama vya Siasa, Wakuu wa Mikoa na Wilaya za Pemba, Maafisa Wadhamini wa Wizara mbalimbali, sambamba na Wakurugenzi kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.

Kitengo cha Habari

Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar

1 June,2022.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.