Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Lela Muhamed Mussa akiwa katika mkutano wa "UN Transforming Education Summit 2020" unaofanyika Paris Nchini Ufaransa.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Lela Muhamed Mussa amehudhuria "UN TRANSFORMING EDUCATION SUMMIT 2022" huko Paris nchini Ufaransa.
Katika mkutano huo wa siku nne uliohudhuriwa na mawaziri mbalimbali duniani utajadili na kupitisha agenda mbali mbali kwa ajili ya mpango wa Elimu wa miaka mitano kwautakaotekelezwa na UNESCO.
Katika picha ni ya baadhi ya wadau wa mkutano wa wanufaika wa GPE ikiwemo Tanzania bara na Zanzibar wenye lengo kuu la kuangalia jinsi nchi hizo zinavyonufaika na ufadhili wa GPE .
Kwa Zanzibar GPE imefadhili miradi mbalimbali kama Kusimamia uendeshaji wa Vituo vya Tucheze Tujifunze,
Kupatiwa vifaa vya kujifinzia na kufundishia, Kuwalipa maposho walimu wa vituo vya TuTu
Kujenga, kukamilisha na kukarabati madarasa na vituo vya TuTu,
Kuwapatia mafunzo ya kuinuwa kiwango cha ufundishaji walimu wa madarasa ya Maandalizi na Vituo vya TuTu na kuanzisha ujenzi wa vituo vya TuTu kwa Unguja na Pemba.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Lela Muhamed Mussa akiwa na GPE Executive Director Charles North katika mkutano wa Wadau wa Wanufaika wa GPE ambapo ni muendelezo wa EDUCATION TRANSFORMATION PRE SUMMIT Paris Ufaransa.
No comments:
Post a Comment