
Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba, Mhe. Bruno Rodrieguez Parrilla amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kuanzia tarehe 29 hadi 30 Juni 2022.
Akiwasili katika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Mhe. Perrilla amepokelewa na Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula.
Wakati wa mapokezi hayo, Mhe.
Balozi mulamula ameeleza madhumuni ya ziara hiyo ni kuimarisha na kukuza ushirikiano
wa kihistoria ulioasisiwa na Wasisi wa mataifa hayo mawili, Hayati Baba wa
Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Hayati Fidel Castor aliyekuwa Rais wa
kwanza wa Taifa la Cuba.
Tanzania na Cuba zimeendelea
kushirikiana katika maeneo ya afya, elimu, viwanda, na biashara. Pamoja na
maeneo hayo serikali hizo mbili zinatarajia kufungua maeneo mapya ya
ushirikiano katika sekta za Kilimo, utalii, ushirikiano katika usimamizi wa
masuala ya zimamoto na uokoaji, utamaduni na michezo.
Aidha, akiwa nchini Mhe. Parrilla
pamoja na mambo mengine atakutana kwa mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Mhe. Liberata Mulamula na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na
Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji.
No comments:
Post a Comment