
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akizungumza na waandaaji wa tamasha la Nandete Majimaji Festival la kutangaza utalii wa utamaduni na malikale, katika kikao kilichofanyika ofisini kwake jijini Dodoma leo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akizungumza na waandaaji wa tamasha la Nandete Majimaji Festival la kutangaza utalii wa utamaduni na malikale, katika kikao kilichofanyika ofisini kwake jijini Dodoma leo. Kulia ni Mbunge wa Kilwa Kaskazini Mkoani Lindi, Mhe. Francis Ndulane.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na waandaaji wa tamasha la Nandete Majimaji Festival la kutangaza utalii wa utamaduni na malikale, katika kikao kilichofanyika ofisini kwake jijini Dodoma leo. Wa tatu kutoka kulia ni Mbunge wa Kilwa Kaskazini Mkoani Lindi, Mhe. Francis Ndulane.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary
Masanja (Mb) amesema Wizara ya Maliasili na Utalii iko tayari kutoa ushirikiano
kwa wadau wanaofanya jitihada za kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kuandaa
matamasha ya kutangaza utalii wa utamaduni na malikale.
Ameyasema hayo leo ofisini kwake jijini Dodoma
alipokutana na waandaaji wa tamasha la Nandete Majimaji Festival
litakalofanyika kuanzia tarehe 13 mwezi Agosti 2022 na kumalizika 15 mwezi
Agosti 2022 katika Kata ya Kipatimo
Kijiji cha Nandete Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi.
Tamasha hilo lenye kauli mbiu ya “Majimaji
Tujiandae Kuhesabiwa”litahusisha mashindano ya mbio, mashindano ya
mpira wa miguu na mashindano ya ngoma za asili ambapo washindi watapewa zawadi
mbalimbali.
No comments:
Post a Comment