Habari za Punde

BRELA NA NIDA KUBORESHA HUDUMA

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu  (Sera, Bunge na Uratibu) Bwa. Kaspar Mmuya  (wa kwanza kushoto) akizungumza katika  kikao  cha Makatibu, Wakuu wa Taasisi kujadili utekelezaji wa Mkataba wa Huduma kati ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)  na Wakala wa Biashara na Leseni (BRELA) anayefuata ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Maduhu Kazi katika  Ukumbi wa Ofisi hiyo  Jijini Dodoma.

Na Mwandishi wetu- Dodoma

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu Bwa. Kaspar Mmuya amesema uboreshwaji wa huduma zinazotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Wakala wa Biashara na Leseni (BRELA) zitasaidia wananchi kupata huduma mbalimbali na wawekezaji kuwekeza kwa wingi Nchini.

Naibu Katibu Mkuu huyo ameyasema hayo  Jijini Dodoma  wakati wa kikao cha Makatibu na Wakuu wa Taasisi kujadili utekelezaji wa Mkataba wa Huduma kati ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)  na Wakala wa Biashara na Leseni (BRELA).

Amesema  kutatuliwa kwa changamoto zinazokabili mamlaka hizo kunatoa fursa kwa wafanyabiashara  kuanzisha bishara zao, viwanda kwa mujibu wa sheria hivyo kuongeza pato la mtu mmoja mmoja hadi Taifa kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.