Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Atembelea Maonesho ya Wajasiriamali Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakipata maelezo ya Bidhaa za Vifuu kutoka kwa Mwakilishi wa Kikundo cha Wajasiriamali cha Kiumbe Mzito kutoka Masingini Bi.Mwanaid Maneno, wakati akitembelea maonesho ya Wajasiriamali yalioandaliwa katika viwanja vya Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Unguja, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, Mama Mariam Mwinyi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, wakimsikiliza Mwakilishi wa Kikundi kutoka Burundi Bi. Chantal Birarondekwa, wakati akitembelea maonesho ya bidhaa za Wajasiriamali mbalimbali yaliyofanyika katika viwanja vya Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Unguja, wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, Mama Mariam Mwinyi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said,na (kulia kwa Rais) Naibu Katibu Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw. Stephen Mlote, wakimsikiliza Mwakilishi wa Kikundi Nia Safi Women Group.Bi. Neema Batraham, wakati akitembelea maonesho ya bidhaa za Wajasiriamali mbalimbali yaliyofanyika katika viwanja vya Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Unguja, wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.