Habari za Punde

MATUKIO MBALIMBALI BANDA LA WIZARA YA FEDHA SABASABA

Naibu  Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Jenifa Omolo (Kushoto) akiongea na Mstaafu Bi Sura Rwiza (kulia) aliyefika kuhakikiwa katika Banda la Wizara kwenye Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara Dar Es Salaam (TanTrade), Jijini Dar Es Salaam. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Benny Mwaipaja.
Wanafunzi kutoka  Ruangwa mkoani Lindi walipotembea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango kwenye Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (TanTrade), Jijini Dar Es Salaam
Mkurugenzi wa SELF MICROFINANCE, Bw. Mudith Cheyo, akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Tehama Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Zuberi Msisi, kwenye Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (TanTrade), Jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na  Utalii  Pro. Eliamani Sedoyeka (Kulia) akifurahia jambo baada ya kupata Elimu kutoka kwa maafisa wa Wizara ya Fedha na Mipango kwenye Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara Dar Es Salaam (TanTrade), Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Benny Mwaipaja
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na  Utalii  Pro. Eliamani Sedoyeka (Kulia) akipokea machapisho kutoka kwa Meneja Masoko na Uhusiano wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Bi. Shamimu Mdee, kwenye Banda la Wizara ya Fedha na Mipango kwenye Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (TanTrade), Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara Dk. Ashatu Kijaji, akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango kwenye Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (TanTrade),kushoto ni Afisa Mapokezi na Katibu Muhtasi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Masia Msuya 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Jenifa Omolo (aliyeshika tuzo) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) ambacho kimeibuka mshindi wa tatu katika tuzo ya jumla kwa upande wa vyuo vya elimu ya juu vinavyoshiriki Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Tantrade).  Kutoka kulia ni Afisa Uhusiano wa  Chuo hicho Bi Sarah Goroi, Afisa Uhusiano Bw. Anold Kavishe na   kushoto  ni Afisa Masoko Benadetha Inyasi

Naibu Katibu Mkuu wizara ya Fedha na Mipango Bi. Jenifa Omolo akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Takwimu Msaidizi Ofisi ya Taifa ya Takwimu kutoka kulia ni  Bi Neema Madembwe Kushoto kwake ni Afisa Maktaba Mkuu Bi Mwanaabu Ngulumbi alipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango kwenye Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara Dar Es Salaam (TanTrade), Jijini Dar Es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu wizara ya Fedha na Mipango Bi. Jenifa Omolo akizungumza na Afisa Udahili wa Chuo cha Mipango ya maendeleo Vijijini (IRDP) Dkt Maclean Mwamlangala (Kushoto)  kulia ni Afisa na Uhusiano Bi Stellah Masanja alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango kwenye Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara Dar Es Salaam (TanTrade) Jijini Dar Es Salaam

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.