Habari za Punde

WIZARA YA AFYA YAZUNGUMZA NA BALOZI WA MAREKANI NCHINI TANZANIZ.

Waziri wa Afya Zanzibar Mhe .Nassor Ahmed Mazrui akizungumza na Balozi wa Marekani Nchini Tanzania  Dkt. Donald Wright na ujumbe wake walipofika Ofisini kwake kujadiliana mambo mbalimbali yatakayopelekea kukua kwa sekta ya Afya  Zanzibar.

Na Kijakazi Abdalla                      Maelezo    14/07/2022

Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui ameyaomba mashirika ya Marekani kuisaidia Zanzibar katika kuwapatia vifaa na elimu ya afya ili kutokomeza vifo  vya mama na mtoto ifikapo mwaka 2030.

 

Waziri Mazrui ameyasema hayo huko Ofisi kwake Mnazimmoja wakati akizungumza na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Donald Wright.

 

Aidha amesema Zanzibar  inatarajia kupunguza vifo vya mama na mtoto na  kuhakikisha ina kuwa na uzazi wa mpango kwa kina mama ili kuzaa  watoto wa wenye afya na siha.

 

Vilevile amesema kutokana na changamoto hizo  wizara inajenga hospitali za Wilaya na Mkoa ambazo zitakuwa na sehemu maalum ya akinamama na watoto ambapo kutawezesha kupunguza vifa vitokanavyo na uzazi. i

 

Hata hivyo amesema Wizara ya Afya wataanza kupita nyumba kwa nyumba ,masokoni na sehemu mbalimbali   katika kampeni ya chanjo ya uviko 19.

Vilevile Waziri Mazru amesema kupitia jitihada za Serikali na  wadau mbalimbali wanaosaidia katika sekta ya afya zimewea kupunguza kwa kiasi kikubwa mradhi ya malaria na HIV.

 

Kwa upande wake Balozi wa Marekani nchini Tanzania Donald Wright ameeisifu Wizara ya Afya kwa jitihada za kupunguza maradhi ya uviko 19 Zanzibar  pamoja na maradhi ya malaria.

 

Aidha amuhakikishia Waziri wa Afya kwa kupitia Serikali yake ya Marekani itahakisha Zanzibar inaondikana na changamoto mabalimbali za maradhi.

“Tutazidi kuunga mkono Serikali ya Zanzibar ili kuhakikisha tuondosha changamoto za maradhi”alisisitiza Balozi Donald Wrght.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.