Habari za Punde

Kamati ya Baraza la Wawakilishi yaendelea na ziara kukagua miradi

Mwenyekiti wa kamati ya Baraza la Wawakilishi ya kusimamia Ofisi za viongozi wakuu wa kitaifa Mhe. Machano Othman Said  akiwapatia maelekezo  watendaji wa kituo cha uwezeshaji Kwa watu wenye ulemavu Kilichopo Mombasa  Magereza  mara alipofika katika kituo hicho  na wajumbe wake kuangalia miradi iliyo chini  ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa  Rais. PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR.

Waziri wa Nchi (AMKR) Mhe. Harusi Said Sleiman akiangalia  keki iliyotengenezwa na Vijana wa  kituo cha mafunzo ya upishi  kilichopo chini ya Baraza la Taifa   la watu wenye ulemavu  (NOAH TRAINING CENTRE ) wakati wa  ziara ya kamati ya Baraza la Wawakilishi ya kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu  kutembelea miradi ya Ofisi ya makamo wa Kwanza wa Rais   huko Mombasa Magereza  . PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR.

 

Kamati  ya Baraza la Wawakilishi ya kusimamia Ofisi za viongozi wakuu wa kitaifa wakiangalia  shamba liliokua likichimbwa kifusi likiwa katika hatua za urejeshwaji wa Ardhi kwaajili ya Matumizi mengine huko Mwera Pongwe wakati wa ziara ya kamati hiyo kuangalia miradi inayotekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais . PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR.
Mmiliki wa Shamba lililokua likichimbwa kifusi Mwera Pongwe Mohammed Hamza akieleza hatua anazochukua Kurejesha Ardhi baada ya Uchimbaji ,wakati alipotembelewa na Kaamati  ya Baraza la Wawakilishi ya kusimamia Ofisi za viongozi wakuu wa kitaifa Ikiwa ni muendelezo wa ziara ya kamati hiyo kuangalia baadhi ya miradi inayotekelezwa na Afisi ya Mamkamu wa Kwanza wa Rais. PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR.
Mkurugenzi Mkuu mamlaka ya Usimamizi wa mazingira Sheha Mjaja akielezea kuhusu urejeshwaji wa ardhi baada ya kuchimbwa mchanga  ,  wakati wa Ziara ya Kamati ya Baraza la Wawakilishi ya kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa kitaifa kuangalia shamba la heka 9 lililokua likichimbwa fusi linalomilikiwa na Mohammed Hamza huko mwera pongwe. PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR
Kamishna Mkuu wa  Mamlaka ya  na Kudhibiti  na Kupambana  na Dawa za kulevya Kanal  Burhani  Zuberi  Nasoro akielezea kuhusu ufugaji wa kuku wakati waliopotembelewa na Kamati ya Baraza la Wawakilishi ya kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa kitaifa kuangalia maendeleo ya miradi katika kituo cha kurekebisha tabia kwa Vijana walioathirika na Madawa ya kulevya  huko  Kidimni Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja . PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR.

Kaamati  ya Baraza la Wawakilishi ya kusimamia Ofisi za viongozi wakuu wa kitaifa wakiangalia mashine  ya kunyanyulia gari katika gereji inayoendelea kujengwa katika kituo cha kurekebisha tabia kwa Vijana walioathirika na Madawa ya kulevya Kidimni  wakati wa ziara ya kamati hiyo kuangalia miradi inayosimamiwa na Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais . PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR. 

 Kamati  ya Baraza la Wawakilishi ya kusimamia Ofisi za viongozi wakuu wa kitaifa wakiangalia  Ujenzi wa majengo ya Ofisi katika kituo cha kurekebisha tabia kwa Vijana walioathirika na Madawa ya kulevya Kidimni  wakati wa ziara ya kamati hiyo kuangalia miradi inayosimamiwa na Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais . PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR.

Kamishna Mkuu wa  Mamlaka ya  na Kudhibiti  na Kupambana  na Dawa za kulevya Kanal  Burhani  Zuberi  Nasoro akiwasilisha ripoti ya utekelezaji wa miradi inayotekelezwa na mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya Chini ya Afisi ya Makamu wa kwanza wa Rais wakati walipotembelewa na kamati ya Baraza la Wawakilishi ya kusimamia Ofisi za viongozi wakuu wa kitaifa huko Kituo cha kurekebishia tabia kwa Vijana walioathirika na Madawa ya kulevya Kidimni  Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja . PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR.

Katibu Mkuu Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Dkt Omar Dadi Shajak akitoa neno la shukurani kwa kamati  ya Baraza la Wawakilishi ya kusimamia Ofisi za viongozi wakuu wa kitaifa mara baada ya kukamilisha ziara yao kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa  na Ofisi ya makamu wa Kwanza wa Rais.PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR.
 

Na Rahima Mohamed  Maelezo  10/8/2022

 

Kamati ya baraza la wawakilishi ya kuwashughulikia viongozi wakuu wa serikali imeridhishwa na hatua  zinazochukuliwa na mmiliki wa shamba lililokuwa likichimbwa kifusi katika eneo la Mwera Pongwe kulirudisha katika uhalisia wake na kutumika katika matumizi mengine .

 

Akifanya majumuisho ya kutembelea miradi ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe Machano Othman Said katika ukumbi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira  Marughubi, amesema mmiliki huyo amechukua juhudi kuwa ya kuweza kuanza kuyafukia baadhi mashimo tofauti na baadhi maeneo mengine hawafanyi hvyo . 

 

“Tunampongeza sana mmiliki huyo kwa kufuata matakwa aliyopewa ya serikali ya ya kusitisha uchimbaji katika eneo na kuanza kuyafukia mashimo hayo  ukilinganisha na baadhi maeneo mengine waliyotembelea ambayo hayarudishwi kama yalivyokuwa”, alisema mhe. Machano.

 

Mhe. Machano ameitaka Mamlaka ya Mazingira  kumsaidia mahitaji mmiliki huyo katika kuyafukia mashimo yaliyomo katika shamba hilo ili lirejee katika hali yake ya kawaida kwa urahisi.

 

“Nawaomba  wachimbaji wengine wawapeleke wakajifunze jinsi ya kuirudisha ardhi baada ya matumizi ya uchimbwaji ili kurudisha katika hali yake ya awali kwa ajili ya matumizi mengine” amesisitiza Mwenyekiti huyo. 

 

 

Akizungumzia katika  Kituo cha kurekebisha tabia kwa watumiaji wa dawa za kulevya Kidimni Mhe.  Machano amesema kamati yao inatoa ushirikiano  katika kusaidia  Zanzibar kutokomeza utumiaji wa dawa ya kulevya ambazo zinaleta athari kubwa kwa vijana  ambao ni nguvu ya taifa.

 

 

Aidha kamati hiyo imesisitiza kuwepo na uwiano wa jinsia katika vituo vya kurekebisha tabia kutokana na idadi ndogo ya wanawake waliofika kupata huduma katika vituo hivyo.

 

 

Nae Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais Harus Said amemtaka mmiliki  huyo kuwa karibu na watendaji  wa mazingira ili kupata miongozo a itakayomsaidia kuirudisha eneo hilokuwa katika hali ya kawaida pamoja na kumpongeza kwa hatua hiyo.

 

 

Waziri huyo amesema ziara hiyo itasaidia kufanya tathmini na kugundua changamoto zilizopo na kuwashauri njia ambazo zitakazosaidia ili kuhakikisha miradi inafikia malengo yaliyokusudiwa.

 

Nae mmiliki wa shamba hilo Muhamad Hamza ametumia gharama kubwa za kufukia eneo hilo hivyo  ameiomba Serikali imsaidie kukamilisha ufukiaji ili liendelee kutumika kwa matumizi mengine.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.