Habari za Punde

Mkutano kuzungumzia Maradhi yasiyoambukiza kwa nchi za Afrika Mashariki wafanyika Zanzibar

Baadhi ya Wajumbe waliohudhuria katika Mkutano wa Siku Mbili kuzungumzia Maradhi mbalimbali  yasioambukiza pamoja na Uviko 19 kwa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika katika Ukumbi wa  Hoteli ya Verde Maruhubi Zanzibar.

 

Mkurugenzi wa Kituo Cha Afrika cha Usimamizi wa Udhibiti na Uzuizi wa Magonjwa (CDC)Dkt,Ahmed Ubwe akitoa hotuba katika Mkutano wa Siku Mbili kuzungumzia Maradhi mbalimbali  yasio ambukiza pamoja na Uviko 19 kwa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika katika Ukumbi wa  Hoteli ya Verde Maruhubi Zanzibar.
Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui akisisitiza jambo wakati akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Mkutano wa Siku Mbili kuzungumzia Maradhi mbalimbali  yasio ambukiza pamoja na Uviko 19 kwa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika katika Ukumbi wa  Hoteli ya Verde Maruhubi Zanzibar.

Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Mkutano wa Siku Mbili kuzungumzia Maradhi mbalimbali  yasio ambukiza pamoja na Uviko 19 kwa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika katika Ukumbi wa  Hoteli ya Verde Maruhubi Zanzibar.

Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui(katikati)akiwa katika Picha ya pamoja na Viongozi na wajumbe waliohudhuria katika Mkutano wa Siku Mbili kuzungumzia Maradhi mbalimbali  yasioambukiza pamoja na Uviko 19 kwa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika katika Ukumbi wa  Hoteli ya Verde Maruhubi Zanzibar.

 

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

NA SABIHA KHAMIS MAELEZO ZANZIBAR              

 

Waziri wa Afya Mh. Nassor Ahmed Mazrui amesema Shirika la Udhibiti na Usimamizi wa Magonjwa  ya Mripuko CDC wameihakikisha Sekta ya Afya kuwa  wataendeleza ushirikiano na nchi za Afrika Mashariki ili kuweza kujikinga na maradhi ya mripuko ikiwemo Kipindupindu ,Uviko- 19 na  Ebola.

 

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano  uliowashirikisha Mawaziri wa wizara ya Afya kutoka nchi mbali mbali  za Afrika Mashariki,  huko ukumbi wa Hotel ya Verde Mtoni Zanzibar, Waziri Mazrui amesema mashirikiano yaliopo kati  yao na shirika hilo yatasaidia kuyapatia ufumbuzi  maradhi hayo.

 

Aidha amesema kupitia mkutano huo utasaidia  kujenga mfumo mpya wa kuimarisha mashirikiano kati yao na umoja wa nchi za Afrika Mashariki  katika sekta ya Afya .

 

Alifafanua kuwa  Mkutano huo  utawanufaisha na  kuwapatia maudhui mazuri watendaji wa Sekta ya  Afya ili kuweza kukabiliana na maradhi hayo pindi  yanapotokezea katika  nchi zao.

 

 “azma ya mkutano huu ni kuziwezesha  Nchi za Afrika Mashariki  kuweza kujikinga na maradhi ya mripuko kutoka nchi moja kwenda nyengine” alisema Waziri Mazurui.

 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Udhibiti na Usimamizi wa Magonjwa ya Mripuko (CDC) Dk. Ahmed Ubwe amesema wapo tayari kufanya kazi  kwa mashirikiano kati yao na Nchi Jirani za Afrika Mashariki ili kuwasaidia kujikwamua  katika maradhi hayo.

 

 

Mkutano huo ni wa siku mbili ukiwashirikisha wadau wa Afya kutoka Nchi Mbalimbali  za Afika Mashariki ikiwemo  Kenya, Rwanda, Burundi, Somalia na nchi nyengine jirani.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.