Habari za Punde

Naibu Waziri Maryprisca Mahundi Atoa Siku Saba Usambazaji wa Maji Kijiji cha Msomera.

NAIBU Waziri wa Maji MarryPrisca Mahundi akizungumza mara baada ya kukagua  mradi wa maji katika Kijiji cha Msomera Kata ya Misima wilayani Handeni ikiwemo kutembelea tenki lenye uwezo wa kuhifadhia maji lita 167,000 unaotekelezwa na Serikali ili kuhakikisha wananchi waliohamia kutoka wilaya ya Ngorongoro wanapata huduma ya maji safi na salama.

Na Oscar Assenga, Handeni

NAIBU Waziri wa Maji Marry Prisca Mahundi ametoa siku saba kwa Meneja wa Ruwasa wilaya ya Handeni Mhandisi Hosea Joseph kuhakikisha anamsimamia mkandarasi wa Kampuni ya Mponela Dicksona Mwipoo anayetekeleza mradi wa maji katika Kijiji cha Msomera wilayani humo kuhakikisha maji yanafika kwenye tenki na kuyasambaza kwa wananchi.


Agizo la Naibu Waziri huyo alilitoa leo wakati wa ziara yake ya kukagua mradi wa maji katika Kijiji cha Msomera Kata ya Misima wilayani Handeni ikiwemo kutembelea tenki lenye uwezo wa kuhifadhia maji lita 167,000 unaotekelezwa na Serikali ili kuhakikisha wananchi waliohamia kutoka wilaya ya Ngorongoro wanapata huduma ya maji safi na salama.


Alisema kwamba thamani ya hilo tenki ni kuhakikisha linatoa maji na yapelekwa kwa wananchi waliopo kwenye Kijiji hicho ili kuweza kuwaondolea changamoto ambazo wanakumbana nazo kusaka huduma hiyo muhimu kwa maendeleo yao na jamii zinazowazunguka.


Aidha alisema wao kama Wizara ya Maji mahali popote wanapoona wananchi wanakwenda kujenga kuishi wanahitajika kupatiwa huduma ya maji na kwa hapo Msomera maji yalikuwa yanapatikana kwa wingi kwa jitihada ambazo zimefanywa na Tanga Uwasa na Ruwasa.


“Niwapongeze Ruwasa ambao wanasimamiwa na Mhandisi Upendo Omari ambaye anafanya kazi nzuri sana hapa tulipo kuna tenki kubwa ambalo lililetwa kutoka nje lengo kuhakikkisha jamii ya msomera inapata maji toshelevu na kwa kupata tenki hili visima vilivyochimbwa hapa vinakwenda kutumika vizuri”Alisema


Naibu Waziri huyo alisema kuna kisima ambacho kinatoa maji mengi na wanategemea ndani ya wiki moja kutoka leo hiikitaanza kusafirisha maji kutoka eneo hilo na kwenda kwenye tenki na baadae usambazaji wa  maji kwa wananchi wataohamia hapa Msomera wanapata huduma ya maji.


“Niwahakikishie kama Serikali kupitia Wizara ya Maji muwe na uhakika mtapata maji kwa matumizi ya majumbani ya uhakika na jamii ina mifugo kwa sababu ya hilo tumejenga maeneo ya kunyeshea mifugo msomera matatu ili kuhakikisha wanyama wanapata maji ya kutosha na tunatambua kenye kundi hili kuna wakulima tayari waziei wa Kilimo atakuja lengo la kuhakikisha pia tunapata wakulima kupitia kilimo cha Umwagiliaji”Alisema Naibu Waziri huyo.


Alisema kwa sababu unjengeji wa nyumba unendelea katika eneo hilo watendelea usambaji wa maji na wanancji wanaendelei kupata maji karibu kwa sababu ujengeji nyuma unaendeleo kusambaa wengine watajikuta wanakuwa mbali na vichoeta maji vyao  watawafuata walipo lengo kuhakikisha maji yanapatikana kwa wingi kwa wananchi.


Hata hivyo alisema kwamba maji yakishafika kwenye tenki yatakwenda kwenye usambazaji wa vichotea maji na kwa wananchi watakaokuwa na uhitaji wa kuyavuta kwenye majumba yao watapewa vigezo vya na masharti nafuu ili waweze kuvuta maji,


“Lakini nitoe wito kwa wakandarsi wote ambao mnapewa kazi nchi mhakikisha mnafanya kazi kwa kujituma bila kuangali malipo yamelipwa kwa wakati au yamechelewa huyu mkandarsi hapa amefanya kazi nzuri tutaendelea kufanya naye kazi Wizara ya maji ipo chini ya Waziri Jumaa Aweso na Rais Samia Suluhu imedhamiria kuhakikisha inamtua mama ndoo kichwani ili waweze kufanya shughuli nyengine za kuchangia kwenye pato la Taifa kwa kufanya shughuli za uzalishaji “Alisema


Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Omari alimueleza Naibu Waziri huyo kwamba wamepokea maelekezo hayo na wao watahakikisha kwamba ndani ya siku tatu wananchi wa eneo hilo wanapata maji.


Akizungumza katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya ya Handeni Siriel Mchemba alisema kuwa kabla ya kuingia Serikali ya awamu ya sita hali ya upatikanaji wa maji ili kuwa chini ya asilimia 34 ambapo ndani ya kipindi cha mwaka mmoja hali ya upatikanaji wa maji umefikia asilimia zaidi ya asilimia 50.


Aidha alisema Wilaya hiyo imefanikiwa kupata zaidi ya Bil 10 ambapo bil 1 inatokana na fedha zitokanazo na uvico ambzo kwa ajili ya Handeni Mjini na Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kwa ajili ya kuondoa tatizo la maji ambalo lilikuwa linaikumba Wilaya hiyo.


Kwa upande wake Meneja wa Ruwasa Wilaya ya Handeni Hosea Joseph alimuhakikishia Naibu Waziri wa Maji kuwa amepokea agizo la kumsimamia Mkandarasi Mponela Construction and co,ltd anaetekeleza ujenzi wa mradi wa maji Kijijini hapo  kuwa utamalizika kwa wakati kama agizo lilivyotolewa.


Hata hivyo alisema mbali ya agizo hilo la siku saba alisisitiza kutokana na umuhimu wa huduma hiyo ya maji atahakikisha ndani ya siku tatu wananchi wa kijiji hicho watakuwa wanapata huduma hiyo ya maji ili kuondoa kero iliyopo ndani ya makazi hayo ya wananchi waliohamia katika eneo hilo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.