Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi atoa mkono wa pole kwa familia ya Marehemu Hajjat Akiba Rajab

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ya kumuombea Marehemu Hajjat Akiba Rajab aliyefariki Madina Nchini Saudi Arabia, baada ya kumaliza kwa Ibada ya Hijja, ikisomwa na Sheikh Abdalla Talib.(kushoto kwa Rais) na (kulia kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria,Utumishi na Utawala Bora Mhe.Haroun Ali Suleiman, baada ya kutowa Mkono wa Pole kwa Familia ya Marehemu Fuoni Wilaya ya Magharibi “B” Unguja jana 5-8-2022.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akitowa mkono wa Pole kwa Familia ya Marehemu Hajat Akiba Rajab, aliyefariki katika Mji wa Madina Nchini Saudi Arabia, baada ya kukamilisha Ibada ya Hijja, alipofika nyumbani kwa Marehemu Fuoni Wilaya ya Magharibi “B”Unguja jana 5-8-2022.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akitowa mkono wa pole kwa Mume wa Marehemu Hajjat Akiba Rajab, aliyefariki Madina Nchini Saudi Arabia baada ya kukamilisha Ibada ya Hijja, Sheikh. Abdulrahaman Saleh alipofika nyumbani kwa marehemu Fuoni Wilaya ya Magharibi “B” Unguja kutoa mkono wa pole kwa familia ya marehemu jana 5-8-2022.(Picha na Ikulu) 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.