Alhaj Dk. Mwinyi amesema hayo katika salamu zake kwa Waislamu baada ya kukamilisha Ibada ya Sala ya Ijumaa iliofanyika Masjid Qubba Kwa Boko Mkoa Mjini Magharibi.
Amesema Dunia iniatambua Kalenda ya Hijria ambapo waislamu hupata fursa ya kuadhimisha mwaka mpya w akiislamu, hivyo akatumia nafasi hiyo kuipongeza Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar kwa kuja na utaratibu wa kuadhimisha Kalenda hiyo.
Alhaj Dk. Mwinyi alisema Serikali imeridhia maombi ya waislamu ya kuifanya siku hiyo kuwa ya mapumziko kitaifa kama ilivyo siku ya mwaka mpya wa Miladia.
Aidha, Alhaj Dk. Mwinyi aliwataka waislamu kuzingatia kwa kina umuhimu wa kufunga siku ya Ashuraa, ikiwa ni funga yenye fadhila kubwa katika mwezi huu wa Muharam.
Nae, Katibu Mtendaji Ofisi ya Mufti wa Zanzibar Sheikh Khalid Ali Mfaume aliwataka waislamu kuendelea kumuombea Dua Rais Alhaj Dk. Mwinyi kwa kuwa ni kiongozi muadilifu na mwenye kutekeleza kwa vitendo ahadi alizoweka.
Mapema, Khatibu wa Sala hiyo ya Ijumaa, Sheikh Hija Suleiman aliwataka waislamu kuendelea kufanya amali njema na kuondokana na maovu, kwa kutambua kuwa mwezi huu wa Muharam ni miongoni mwa miezi minne mitukufu katika uislamu.
Alieleza kuwa kuna fadhila nyingi zinazopatikana katika mwezi huu wa Muharami, ikiwemo ile inayotokana na muislamu kukuthirisha funga , ambapo hupata malipo makubwa.
“Kuna fadhila kubwa kwa kufunga sikukuu hii ya Ashuraa, mja hufutiwa madhambi ya mwaka mzima uliopita”, alisema.
No comments:
Post a Comment