Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Amefungua Maonesho ya Kilimo ya NaneNane Viwanja vya Kizimbani Wilaya ya Magharibi "A" Unguja leo.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikata utepe kuashiria kuyafungua Maonesho ya Kilimo ya NaneNane  katika viwanja vya Kizimbani Wilaya ya Magharibi “A” Unguja leo 8-8-2022 na (kulia kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na (kushoto kwa Rais) Waziri Kilimo,Umwagiliaji,Maliasili na Mifugo Zanzibar Mhe. Shamata Shaame Khamis na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakiwasalimia Wananchi wakati wakitembelea Maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Kizimbani Wilaya ya Magharibi “A” Unguja leo 8-8-2022
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakimsikiliza Mkurugenzi Idara ya Uendeshaji na Utumishi wa Wizara ya Kilimo,Umwagiliaji,Maliasili na Mifugo Zanzibar Ndg. Noha Saleh Said, alipotembelea banda la maonesho la Wizara hiyo, baada ya kuyafungua Maonesho ya Kilimo ya Nanenane yanayofanyika katika viwanja vya Kizimbani Wilaya ya Magharibi “A” Unguja leo 8-8-2022
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi  akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakimsikiliza Bi. Khadija Seif Salum, wakati wakitembelea banda la maonesho la Taasisi ya Pass, baada ya kuyafungua Maonesho ya Kilimo ya Nanenane katika viwanja vya Kizimbani Wilaya ya Magharibi “A” Unguja leo 8-8-2022.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.