Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhew.Dk.Hussein Ali Mwinyi Ameweka Anuwani ya Makazi Nyumbani Kwake Migombani Unguja Leo 22-8-2022

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiweka Nambari ya Anuwani ya Makazi 78 Barabara ya Julius Nyerere katika Makaazi yake Rais wa Zanzibar eneo la Migombani leo 22-8-2022.na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Ujenzi Mawailiano na Uchukuzi Zanzibar.Mhe.Dkt. Khalid Salum Mohammed na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrisa Kitwana Mustafa.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiweka Nambari ya Anuwani ya Makazi 78 Barabara ya Julius Nyerere katika Makaazi yake Rais wa Zanzibar eneo la Migombani leo 22-8-2022.na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Ujenzi Mawailiano na Uchukuzi Zanzibar.Mhe.Dkt. Khalid Salum Mohammed na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrisa Kitwana Mustafa na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi, wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Mhe.Dkt.Khalid Salum Mohammed, akitowa maelezo ya Anuani ya Makaazi, baada ya uwekaji wa anuani hiyo uliofanyika leo 22-8-2022, katika Makazi ya Rais wa Zanzibar eneo la Migomani Wilaya ya Mjini Unguja.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali.(hawapo pichani) baada ya uwekaji wa Anuwani ya Makazi ya Rais wa Zanzibar eneo la Migombani Wilaya ya Mjini na (kulia kwa Rais ) Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Mhe.Dkt.Khalid Salum Mohammed

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk. Hussein Ali Mwinyi amewataka Wazanzibari wote kujitokeza kuhesabiwa katika zoezi la Sensa ya    Watu na Makaazi 2022,  linalotarajiwa kufanyika Agosti 23, 2022.                   

                                                            

Dk. Mwinyi ametoa wito huo katika hafla ya makabidhiano ya  Anuani za Makaazi, hafla iliofanyika katika makaazi ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Migombani, Mkoa Mjini Magharibi.

Amesema Serikali imefikia uamuzi wa kuifanya siku hiyo (Agosti 23, 2020)  kuwa ya mapumziko ili kutoa fursa kwa wananchi wote kuweza kushiki kikamilifu katika zoezi hilo litakalofanyika nchini kote.

Alisema ana furaha kubwa kupokea anuani hiyo na kufanikisha mchakato huo  kwa wakati kabla ya zoezi la sensa na makaazi 2022 kuanza kama ilivyoelekezwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan. 

“............... mimi nitashiriki zoezi hilo na matumaini yangu  Wazanzibari wote watashiriki zoezi hilo na kumalizika kwa salama na amani”, alisema.

Nae, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Dk. Khalid Salum Mohamed  alisema hadi kufikia sasa Wizara hiyo kwa mashirikiano ya karibu na Shirika la Posta Tanzania imefanikiwa kuweka Anuani za Makaazi zipatazo 451,128 Unguja na Pemba, ikiwa ni zaidi ya malengo yaliowekwa.

Alisema hatua hiyo ni ya mafanikio kwa kuzingatia kuwa utekelezaji wake umekwenda sambamba na muongozo wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, alielekeza zoezi hilo liwe limekamilika kabla ya zoezi la sensa ya watu na Maakazi kuanza.

Alieleza kuwa kazi iliobaki ni ya uwekaji wa Vibati katika baadhi ya Nyumba na Majengo, na akabainisha zoezi linaloendelea la uwekaji wa nguzo ambapo nguzo 17,000 zinatarajiwa kuwekwa katika mitaa mbali mbali Unguja na Pemba.

Katika hafla  hiyo ambapo Viongozi mbali mbali wa Serikali walishiriki , akiwemo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita pamoja na Mkuu wa Mkoa Mjini Magahribi Idrissa Kitwana Mustafa; Rais Dk. Mwinyi alikabidhiwa Anwani ya Makaazi Nyumba nambari 78, Wadi ya Migombani, Wilaya Mjini Zanzibar katika Mtaa wa Julius Nyerere Road.

Operesheni ya uwekaji wa Anuani ya Makaazi  ilizinduliwa nchini mnamo  Februari 8, 2022 na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, ambapo  kwa upande wa Zanzibar ilizinduliwa na Makamo wa Pili wa Rais Hemed Suleiman Abdulla Februari 20,2022.

Imetayarishwa na Idaya ya Mawasiliano

Ikulu Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.