Na
Mwandishi Wetu, Zanzibar.
SERIKALI
ya Mapinduzi ya Zanzibar [SMZ], kupitia kwa Mkuu wake wa Wilaya ya Mjini
Mh.Rashid Simai Msaraka imesema inatambua na juhudi za tamasha la Reggae
Zanzibar katika kuleta tija ya kukuza uchumi Visiwani Zanzibar.
Mh.Msaraka
amesema hayo katika mkutano maalum wa Waandisshi wa Habari na Wasanii wa Reggae
wanaoshiriki msimu wa Nne wa tamasha la Muziki wa Rege [Zanzibar Reggae
Festival] linalofanyika kwa siku mbili Agosti 5-6, ndani ya Mambo Club, Mji
Mkongwe.
‘’Serikali
inatambua umuhimu wa matamasha ya muziki ndani ya Zanzibar, pia mziki wa Reggae
tunataka uwe mkubwa na kuendelezwa kama Sera ya Serikali na Chama chetu cha
Mapinduzi [CCM] sababu yanaleta tija katika uchumi na kukuza ajira kwa vijana
na jamii kwa ujumla, Na kuongeza kuwa, wanaamini Tamasha hilo
litakuwa kubwa na miongoni mwa matamasha yatakayochangia uchumi Visiwani hapa.
alisema Mh. Msarika
Aidha,
amewataka Watu waachane na imani potofu kwa jamii ya Kirasta na muziki wa
Reggae, kwani ni kama imani nyingine, zaidi amewataka kuzingatia sheria za nchi
zilizopo,
Hata
hivyo, amewataka watu wenye imani ya Kirasta kusaidiana na Serikali kufichua
wanaotumia jina la ‘RASTA’ vibaya kama kuiba, kubaka ama kufanya uhalifu hali
inayopelekea taswira mbaya kwa jamii na Serikali.
‘’Naomba
tuendelee kuwa wa mfano, ikiwemo kushirikiana na Serikali, kakatika kufichua
masuala ya kialifu, tukemeane wenyewe kwa wenyewe, ilikulinda imani hii na sie
Serikali milango iko wazi kuendelea kushirikiana.
..watu
wanaotaka kujua mengi kuhusu Rasta waweze kujiunga na Rasta wenyewe, ambao Wana
umoja wao, kwani pia wanaubiria amani
na upendo.’’ Alisema Mh. Msaraka.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Tamasha hilo, Said Omary Hamad ‘Side Rasta’ ameishukuru
Serikali kwa kuendelea kuunga mkono uwepo wa tamasha hilo huku akiomba wadau
mbali mbali waendelee kujitokeza kudhamini.
‘’Tunaomba
wadau mbali mbali kujitokeza kudhamini tamasha la Reggae Zanzibar, kwani uwepo
wa tamasha ni ukuaji wa uchumi wetu, milango ya udhamini ipo wazi’’ alieleza
Side Rasta.
Aidha,
amewataja Wasanii wa muziki wa Reggae kwenye tamasha hilo kuwa ni Ras Gumbo,
Nile Dawta (Nairobi Kenya), Mr Kamanzi, Mack El Sambo (DRC Congo), Brasto Imva
(Malawi ), Ras Coco (Zanzibar) na Zion Rebels (Ethiopia) na wengineo.
No comments:
Post a Comment