Habari za Punde

TAMWA-ZNZ Yataka Kuwepo kwa Mazingira ya Usawa wa Kijinsia Tume ya Uchaguzi ZEC

Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi  ya Zanzibar Ndg.Khamis Kona Khamis akisistiza jambo na Mkurugeni wa TAMWA-ZNZ Dkt,Mzuri Issa katika nje ya tume hiyo mara baada ya kumaliza kwa mkutano wa majadilino.

Mkuu wa miradi TAMWA-ZNZ Ndg.Ali Mohamed akisisitiza jambo wakati alipokua akichangia katika mkutano huo.

Picha ya pamoja ya washiriki wa mkutano huo mara baada ya kumalizika katika jingo la Tumeya uchaguzi Zanzibar (ZEC) Maisara mjini Unguja.

Na.Muhammed Khamis,TAMWA-ZNZ

Chama cha waandishi wa habari wanawake TAMWA-ZNZ kimesema  wakati umefika kwa Tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC) kuhakikisha kinaweka mazingira ya usawa wa kijinsia katika utekelezaji wa shughuli zao mbali mbali zikiwemo za usimamizi wa chaguzi na nyenginezo.

 

Kauli hiyo  imekuja  kufuatia mkutano malumu wa majadiliano baada ya kumalizika kwa mkutano  awali uliofanyika mwezi septemba mwaka jana na kupeana na majukumu kwa pande zote mbili kupitia  sera jinsia ya mjumuisho kwa ajili ya kutazama uwepo wa mazingira ya  usawa wa kijinsia katika muundo wa tume hiyo na utendaji wa kazi zake.

 

Akizunguma katika mkutano huo Mkurugenzi wa Chama hicho Dkt,Mzuri alisema ushiriki wa wanawake katika shuhuli za tume hiyo utaleta mwanga zaidi na hatikame kuwafanya wanawake wengi waweze kufikia malengo yao yakiwemo ya kuwa viongozi.

 

Alisema kwa miaka mingi katika kazi za tume hiyo kumeonekana  wanaume wengi ndio wanaoshiriki shughuli za tume zikiwemo za usimamizi wa chaguzi zinazofanyika huku idadi kubwa ya ushiriki ikionekana kuwa ya wanaume na wanawake kuwa nyuma licha ya kuwa ndio wenye idadi kubwa katika kila chaguzi zinazofanyika.

 

Alisema iwapo wanawake wengi watashiriki katika utendaji wa tume hiyo utapelekea wanawake wengi zaidi kushiriki katika harakati za kuchagua na kuchaguliwa na hatimae idadi kubwa ya wanawake kutumiza ndoto zao za kuw aviongozi itafakiwa.

 

‘’Hata kama ikitokea idadi kubwa ya wanawake hawakuomba nafasi kwenye tume lakini muna wajibu wa kukweka kanuni ambazo zitalazimisha asasi za kiraia kupeleka idadi kubwa ya wanawake katika shughuli za tume zikiwemo zile za usimamizi wa chaguzi zinazofanyika kila baada ya miaka mitano’’aliongezea Dkt,Mzuri.

 

Kwa upande wake  mkuu wa miradi TAMWA-ZNZ Ali Mohamed alisema wakati mabadiliko hayo ya kuleta usawa wa kijinsia  yanaendelea kufanyika kunahitajika kujengwa mazingira lazimisha katika sheria ya msajili wa vyama vya siasa ambayo itaonesha uwepo wa idadi sawa ya ushiriki wa wanawake katika kugombe anafasi za uongozi.

 

Alisema kuwepo kwa sheria hiyo kutapalekea mazingira rafiki kwa wanawake wengi na kuondoa ukandamizwaji ambao kwa miaka mingi wanawake wamekua wakilalamika, na wanadai kuwa hufanywa na watu wenye nafasi za maamuzi kwenye vyama vyao kupitia idadi kubwa ya wagiombea kuwa wanaume na wananwake huwa wachache.

 

Awali Mkurugenzi wa Uchaguzi Tume ya Uchaguzi  ya Zanzibar Khamis Kona Khamis alisema mkutano huo wa majadiliano umekuja wakati muafaka ambapo tume hiyo ipo kwenye mchakato wa kulifganyika kazi suala hilo.

Smbamba na hayo alisema licha ya uwepo wa changamoto za hapa na pale lakini kwa kiasi kikubwa tume hiyo inaendelea kufanyika kazi maswala ya kijinsia na ndio maana baadhi ya wilaya zikiwemo kaskazini Unguja maafisa wote wa tume hiyo ni wanawake.

Pamoja na hayo alisema bado TAMWA-ZNZ kwa kushirikiana na asasi nyengine za kiraia wana wajibu wa kupeleka mapendekezo yao pale wanapoona kuna changangamoto za mifumo na iwapo watafanya hivyo watasaidia sana utendaji kazi wa tume hiyo na kupeleka mbele maendeleo kwa maslahi ya Taifa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.