Habari za Punde

Tangazo la nafasi za masomo kwa fani za afya na uhandisi Ras al Khaaimah

 Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar inatangaza nafasi za ufadhili wa masomo wa Shahada ya Kwanza unaotolewa na Serikali ya Mfalme wa Ras al-Khaimah katika mwaka wa masomo 2022/2023 kwa fani za afya na uhandisi.


Sifa za muombaji


1.   Awe amemaliza kidato cha sita mwaka 2022 kutoka skuli za sekondari zilizopo Zanzibar


2.   Awe amepata ufaulu wa daraja la kwanza katika mitihani ya Taifa ya kidato cha sita iliyofanyika May, 2022 kwa masomo ya Sayansi.


3.   Awe amefaulu mitihani ya Kimataifa yakupima uwezo wa Lugha ya Kiingereza (TOEFL au IELTS)


4.   Awe na Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi


5.   Awe na Paspoti ya kusafiria


6.   Awe na afya njema


7.   Atume maombi yake ya Chuo kupitia tovuti za Vyuo  vifuatavyo:


a.   Ras Al-Khaimah University of Health and Medical Science kwa wanafunzi wa fani za sayansi za afya. Tovuti:www.rakmhsy.ac.ac


b.   American Univesity in Ras Al-Khaimah (AURAK) kwa wanafunzi wa fani za Uhandisi. Tovuti: www.aurak.ac.ac.


Aidha kila muombaji anapaswa kuandika barua za maombi ya nafasi aliyoomba na kuituma kwa Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar akiambatisha:


a)  Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari


b)  Kivuli cha hati ya kusafiria


c)   Kivuli cha cheti au matokeo ya kidato cha sita.


d)  Kivuli cha matokeo ya TOEFL au IELTS


e)  Fomu ya maombi ya kujiunga na Chuo iliyojazwa vyema.


f)     Kivuli cha barua ya udahili wa chuo husika


Maombi ya nafasi hizo za ufadhili wa masomo yawasilishwe katika ofisi za Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu zilizopo kwa Mchina Mwisho mkabala na Jengo la Manispaa ya Magharib B kwa Unguja na Chake Chake Ofisi za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kwa Pemba si zaidi ya tarehe 20/08/2022


Tangazo hili pia linapatikana katika tovuti ya Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu Zanzibar www.zhelb.go.tz


Waombaji wote wanakaribishwa.


 


Ahsanteni

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.