Habari za Punde

Waziri Dkt. Nchemba Aziomba Taasisi za Dini Kumuomba Rais Katika Kutimiza Dira ya Maendeleo

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akicheza wakati wa wimbo wa Jubilei ya Miaka 50 ya Jimbo Katoriki la Singida, wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Singida, Bw. Peter Serukamba, hafla iliyofanyika Mkoani Singida.

Na. Peter Haule, WFM, Singida                                                                                                              

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.Mwigulu Lameck Nchemba ameziomba taasisi za Dini kuendelea kumuombea Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, ili aendelee kuiongoza nchi vizuri na kutimiza dira yake ya uwekezaji katika sekta ya uzalishaji, kutengeneza ajira, kukuza uchumi na kujenga Tanzania yenye umoja.

Dkt. Nchemba alitoa rai hiyo mkoani Singida aliposhiriki katika jubilei ya miaka 50 ya Jimbo Katoriki Singida.

Alisema Mhe. Rais anadhamira ya dhati ya kuwaletea maendeleo wananchi wake, hivyo ni vema kumuombea ili yale aliyodhamiria kwa ajili ya nchi yaweze kutimia.

Aidha alisema kuwa taasisi za Dini zinamchango mkubwa katika kuchochea maendeleo ya jamii katika sekta mbalimbali za maendeleo zikiwemo za afya, maji na elimu hususani maeneo ya pembezoni.

Alisema ni vema taasisi hizo zikaendelea kutimiza jukumu hilo ikiwa ni pamoja na kuhubiri amani na umoja miongoni mwa watanzania.

Alisema kuwa kabla dini hazijashamili katika mkoa huo kulikuwa na vitendo vingi vya kihalifu lakini kwa sasa vitendo hivyo vimepungua, hivyo Serikali haiwezi kubeza jitihada za taasisi za Dini katika jambo hilo.

Aidha alitumia jukwaa hilo kuwahimiza wananchi kuhakikisha wanashiriki katika zoezi la Sensa ya watu na makazi kwa kutoa taarifa sahihi kwa makarani wa sensa, jambo litakaloisaidia Serikali kuweka mipango ya maendeleo kulingana na uhitaji wa wananchi.

Awali Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa Katoriki Jimbo kuu la Dar es salaam, Kardinal Polycarp Pengo, aliwataka viongozi wa kanisa kuwafikiria wengine wenye mahitaji katika kipindi cha miaka 50 ijayo.

Alisema ni kweli Jimbo Katoriki la Singida lilipoanzishwa miaka 50 iliyopita lilikuwa katika hali duni lakini sasa jimbo hilo limekua na kuwa na uwezo wa kuyasaidia majimbo mengine yenye mahitaji pamoja na kushiriki kusaidia jamii

Aidha alisema kuwa mapadri wa mashirika wazawa wa jimbo la Singida wanashiriki kati huduma katika mashirika mbalimbali ndani na nje ya nchi jambo ambalo ni jema kwa kanisa.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mstaafu, Jenerali Venance Mabeyo, wakati wa Jubilei ya Miaka 50 ya Jimbo Katoriki la Singida.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Bw. Peter Serukamba, wakati wa wa Jubilei ya Miaka 50 ya Jimbo Katoriki la Singida.
Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa Katoriki Jimbo kuu la Dar es salaam, Kardinal Polycarp Pengo, akizungumza jambo wakati wa Jubilei ya Miaka 50 ya Jimbo Katoriki la Singida.
Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es salaam Mstaafu Kardinal Polycarp Pengo, (katikati) akiwa katika Jubilei ya Miaka 50 ya Jimbo Katoriki la Singida.
Baadhi ya maaskofu wa Kanisa la Katoriki kutoka Majimbo mbalimbali wakiwa katika Jubilei ya Miaka 50 ya Jimbo Katoriki la Singida.

Baadhi ya Masista wa Kanisa la Katoriki kutoka Majimbo mbalimbali wakiwa katika Jubilei ya Miaka 50 ya Jimbo Katoriki la Singida.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WFM, Singida)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.