Habari za Punde

WAZIRI WA AFYA AFANYA MAZUNGUMZO NA WADAU MBALIMBALI WA AFYA KATIKA KUIMARISHA SEKTA HIYO

Waziri  wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui akizungumza na Wajumbe wa Shrika la Maendeleo D,tree kuhusiana na  uimarishaji  wa  Wahudumu wa Afya wa Kujitolea CHV, walipofika Ofisini kwake Mnazimmoja  kujadili maendeleo ya wahudumu hao. 

Waziri wa Afya Zanzibar Mhe.Nassor Ahmed Mazrui akizungumza na Ujumbe  kutoka uturuki wakishirikiana na Miko wakijadili upatikanaji wa huduma ya  Afya ikiwemo dawa na Vifaa Tiba mara walipofika ofisi kwake Mnazimmoja kujadili upatikanaji wa huduma hizo.

Waziri  wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui akimkabidhi zawadi maalum Mjumbe  wa Shrika la Maendeleo Dtree mara baada ya kujadili uimarishaji  wa  Wahudumu wa Afya wa Kujitolea CHV huko Wizarani kwake Mnazimmja Zanzibar

PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR

Na Rahma Khamis Maelezo     Zanzibar  26/8/2022                                                      

Waziri wa Afya Zanzibar Mhe, Nassor Ahmed Mazrui amesema wataendelea kushirikiana na Mashirika mbalimbali ya maendeleo  ili kuimarisha sekta ya afya nchini.

Akizungumza na washirika wa maendeleo ya afya  D,Tree huko Ofisini kwake  Mnzimmoja mara baada ya kufika na kujadili masuala mbalimbali yanayohusu wahudumu wa Afya ya kujitolea (CHV),  amesema wahudumu hao ni muhimu sana kwani wanaisaidia Wizara katika kuendesha harakati mbalimbali za Kiafya.

Amesema wahudumu wa afya wa kujitolea (CHV ) wanafanya kazi ngumu na kubwa  katika jamii  ikiwemo kuwapatia elimu ya kuimarisha Afya ya mama na mtoto jambo linaloisaidia Wizara  katika kupunguza madhara yatokanayo na uzazi.

Aidha amefahamisha kuwa Wizara imejipanga kuhakikisha kuwa inaimarisha maslahi ya wahudumu hao ili kuwapa moyo Zaidi wa kuendelea kufanya kazi na kuhakikisha  Afya za jamii zinaimarika .

“Baadhi ya wanajamii hawana uwelewa kuhusu maendeleo ya afya ya uzazi  ambapo mama mjamzito huchelewa kufika hospitali na kusababisha ongezeko la vifo vya mama na mtoto,hivyo wahudumu hawa wanajukumu kubwa la kutoa elimu zaid kwa jamii.”alisema Waziri Mazrui

 Nao wajumbe wa Shirika la D,Tree wameishukuru Wizara ya afya kwa ushirikiano wao na kuahidi kuongeza ushirikiano Zaidi katika sekta hiyo ili kupambana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza .

Wakati huohuo Waziri Mazrui alikutana na ujumbe kutoka Uturuki na kujadili kuhusu upatikanaji wa madawa na vifaa tiba ambavyo vitasaidia katika matibabu mbalimbali kwa wagonjwa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.