Habari za Punde

Wenye ulemavu nao watakiwa kushiriki Sensa

 Na Mwashungi Tahir -Maelezo  

 

Watu wenye ulemavu wanahitajika kushiriki kikamilifu katika zoezi la sensa ya watu na makaazi ili serikali kukamilisha sera  maalum ya uhitaji wa watu wenye ulemavu Kwa mipango sahihi ya maendeleo.

 

Akifungua kongamano la  sensa ya watu na makaazi  kwa watu wenye ulemavu katika Ukumbi wa Umoja wa watu wenye ulemavu Kikwajuni Mjini Zanzibar  Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Fedha na mipango Sada Mkuya Salum  amesema ushiriki wa watu hao utaiwezesha serikali kupanga bajeti maalum itakayowasaidia katika nyanja zote ikiwemo elimu afya na uhitaji wa ajira .

 

Aidha Ameitaka jamii kutowaficha watu wenye ulemavu ili kupata kutoa  taarifa zao kwa usahihi ambazo zitaipa chachu serikali kujipanga kikamilifu katika suala zima la maendeleo endelevu kwa wananchi wake.

 

Akitoa shukrani Mwakilishi wa viti maalum kupitia nafasi za watu wenye ulemavu Mwantatu Mbarak Khamis Amesema atahakikisha watu wenye ulemavu wanashiriki zoezi hilo muhimu ambalo litasaidia kutumika kupata fursa mbali mbali na kutambuliwa kitaifa .

 

Wakitoa ufafanuzi juu ya mafunzo hayo Mkurugenzi Idara ya takwimu za kijamii kutoka ofisi ya Mtakwimu Mkuu Zanzibar Fahima Mohammed Issa na Msaidizi wa sensa ya watu na makazi Hamida Suleiman Wamesema mafunzo hayo yatawawezesha kuwasaidia  watu wenye ulemavu kutoa taarifa sahihi ili ziweze kuisaidia serikali katika kupanga mipango maalum ya bajeti yao na kuwawezesha kiuchumi .

 

Kwa upande wao wakufunzi wa mafunzo hayo Wamesema elimu hiyo itawasaidia kuwapa uwelewa zaidi na kuahidi  kuwashajihisha na wengine kushiriki katika zoezi la sensa ya watu na makaazi .

 

 Mafunzo hayo ya siku Moja yenye lengo la kuwahamasisha na kuwapa uwelewa zaidi kwa watu wenye ulemavu katika suala zima la ushiriki wa zoezi la sensa ya watu na makazi .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.