Habari za Punde

Balozi Mulamula Aifariji Familia ya Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akitoa mkono wa pole kwa Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Alhaj Ali Hassan Mwinyi alipomtembelea nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akitoa mkono wa pole kwa Mke wa Rais Mstaafu Mama Khadija, kwa kufiwa na Mtoto wao Marehemu Hassan Ali Hassan Mwinyi aliyefariki 31,Agosti 2022 Zanzibar, alipomtembelea nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akitoa mkono wa pole kwa familia ya Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Alhaj Ali Hassan Mwinyi alipoitembelea familia hiyo kwenye makazi yake Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb.) ametoa pole kwa Familia ya Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Alhaj Ali Hassan Mwinyi kufuatia kifo cha mtoto wake Hassan Ali Hassan  kilichotokea tarehe 31 Agosti, 2022 katika Hospitali Kuu ya Mnazi mmoja, Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.