Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman , akizungumza na wanafunzi na walimu wa Skuli za Mikoa mitano ya Zanzibar pamoja na wananchi mbali mbali huko uwanja wa Amaan Mjini Unguja katika maadhimisho ya miaka 58 ya kilele cha tamasha la Elimu Bila Malipo, yaliyofanyika leo tarehe 23,septemba.
Mhe. Othman alimuakalisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi. ( Picha na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
Na.Kitengo cha Habari OMKR 23.09.2022.
Rais wa Zanzibar na Mwenyikiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Mwinyi, amesema kwamba maendeleo makubwa yamepatikana katika Sekta ya Elimu nchini tangu kutangazwa elimu bila malipo miaka 58 ilyopita.
Mhe.Dk Mwinyi ameyasema hayo katika hotuba
iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman huko Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar
katika maadhimisho ya kilele cha Tamasha
la kutimia miaka 58 ya Elimu bila malipo Zanzibar.
Mhe. Dk . Mwinyi amesema kwamba mafanikio hayo
yametokana na matokeo ya juhudi za Serikali katika utekelezaji wa mkakati wake wa
kuimarisha miundombinu ya upatikanaji wa
huduma hiyo ikiwemo ujenzi wa taasisi za elimu za ngazi mbali mbali.
Amefahamisha kwamba hatua hiyo imepelekea kuongeza fursa za upatikanaji wa elimu kwa
watoto katika ngazi mbali mbali bila ya
ubaguzi wa aina yoyote sambamba na kuongezeka ujenzi wa wa taasisi za elimu kama dhamira ya mapinduzi
ya mwaka 1964 ya kuweka fursa sawa ya elimu kwa wote.
Aidha Mhe. Mwinyi amesema Serikali awamu ya Nane, inaendelea kufidia
michango ya elimu iliyokuwa ikitolewa na wazazi na wanafunzi wote wa skuli za Serikali za
maandalizi hadi sekondari wanaendelea kupatiwa elimu bila kulipa na serikali
ikizipatia skuli nyenzo na vitendea kazi kama vile chaki na madaftari.
Pia Mhe. Mwinyi amesema kwamba
mbali na vifaa hivyo, skuli zote za sekondari za Serikali zinaendelea kupatiiwa
fedha kulingana na idadi ya wanafunzi ili kusaidia uendeshaji wa skuli hizo katika
kipindi hiki ambacho Serikali imechukuwa hatua ya kufuta michango ya wazee
maskulini.
Aidha amesema kwamba kutokana na juhudi za
serikali kutimiza lengo la Elimu bila malipo, idadi ya skuli imeongezeka kwa
kiwango kiukubwa ambapo maandalizi zimefikia 153 kutoka skuli moja kabla ya
mapinduzi , wakati msingi hivi sasa zimefikia 577 na sekondari ni 228 kutoka
tano kabla ya mapinduzi ya mwaka 1964.
Akizungunzia Vyuo Vikuu, amesema
kabla ya Mapinduzi Zanzibar haikua na chuo Kikuu hata kimoja, lakini hivi sasa
vipo vinne vyenye jumla ya wanafunzi 12,527 na pia ipo taasisi ya ufundi Karume na vipo
vyuo vitano vya mafunzo ya amali na
vituo vya Elimu mbadala Unguja na Pemba.
Amesema shabaha ya serikali ni
kutatua changamoto zote zilizopo katika sekta hiyo kwa kuongeza miundombinu ya
kujifunzia na kufundishia ili kufikia azma ya serikali ya kuwa na wasomi
wakaoweza kuongeza idadi ya wataalamu kila fani ili kusaidia ujenzi wa nchi.
Kuhusu maslahi ya waalimu, Mhe.
Mwinyi amesema Serikali imepandisha mishahara ya walimu
kiasi ambacho hata walimu wenyewe hawakuamini ongezeko hilo na kuahidi
kwamba Serikali itaendelea kuangalia maslahi ya wafanyakazi hao kadri
uwezo wa uchumi unavyoruhusu.
Akizungumzia Uchumi wa bluu Dk.
Mwinyi amesema kwamba Serikali ya Awamu ya Nane inaendelea na azma yake ya
kuisimamia kwa vitendo sera ya Uchumi huo
nili kutoa fursa kwa wananchi kuweza kunufaika na rasilimali za bahari.
Ameongeza kuwa, Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Amali ni wadau wakubwa wa kutoa elimu hapa nchini, kwa hivyo wana
wajibu kuungana na Serikali kupitia taasisi mbalimbali kuhakikisha kuwa
marekebisho ya Sera ya Elimu na Mitaala yanazingatia mahitaji ya Uchumi wa
Buluu.
Amefafanua kwamba katika
kuhakikisha hilo, Serikali hivi karibuni itaanza utekelezaji wa Mradi Mkubwa
wenye lengo la kuimarisha Uchumi wa Buluu wa kuwaongeza ujuzi, maarifa na
utaalamu vijana katika Soko la Uchumi huo ambapo utaongeza vyuo vya amali kote nchini, utajenga
Chuo cha Ubaharia, na utaimarisha Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia.
Aidha Mhe. Mwinyi ametoa wito kwa
waalimu kote nchini kwamba ongezeko la mishahara liwe chachu ya kuongeza bidii
katika kutekeleza wajibu na majukumu, ili kuleta mabadiliko ambayo Serikali
inakusudia.
Naye Waziri wa Elimu na Mafunzoya
Amali Zanzibar Mhe. Lela Muhammed Mussa amesema kwamba wizara hiyo itaendelea kusimamia
malengo ya elimu bila malipo katika kuhakikisha kwamba kila mtoto wa Zanzibar
anapata elimu anayostahiki.
Amsema kwamba ni busara kila mmoja
kuhakikisha anashiriki kusimamia sera ya elimu bila malipo sambamba na
kuangalia mwendendo wa dunia katika kuhakikisha kwamba elimu inafanyiwa mageuzi
katika kuhakikisha elimu ya nchi inakwenda na mahitaji .
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na
Maunzo ya Elimu Ali Khamis Juma amsema
kwamba katika jitihada za serikali kuendelea kuimarisha sekta ya elimu na
kufanya mageuzi katika sekta hiyo imeunda kikosi kazi na tayari kinafanya kazi
kubwa ya kupokea maoni ya wadau kuhudu
haja ya mabadiliko katika elimu Zanzibar.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa
Mjini Mgharib akitoa salamu za Mkoa Mkuu wa Wilaya ya Magharib ‘B’ Hamida Mussa
Khamis kwa Niaba ya Mkuu wa ,Mkoa amesema kwamba Mkoa umeridhika na juhudi za
kuatatua changamoto za elimu kwa kujenga miundombinu muhimu ikiwemo madarasa
jambo ambalo litapunguza sana idadi ya wanafunzi madarsani hadi kufikia
45.
Kilele cha Elimu bila Malipo
kutimia mika 58 limeanza kwa tamasha la elimu elimu lilohusisha mashindano ya
michezo mbali mbali ikiwemo mpira wa
miguu na utunzi wa isha pamoja na msaula kadhaa ya kitaaluma amba zawadi mbali
mbali zilitolewa.
Aidha mapema mgeni rasmi alipokea
maandamano ya wanamichezo wanafunzi kutoka Skuli mbali za Unguja na Pemba kwa mikoa yote mitano ya
Zanzibar.
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kupitia Kitengo cha Habari leo tarehe 23.09.2022.
No comments:
Post a Comment