Habari za Punde

Serikali Yasikia Kilio cha Tozo

 

Kamishna Msaidizi - Idara ya uchambuzi wa Sera kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Wiliam Mhoja (kushoto), akitoa ufafanuzi wa tozo ya miamala ya kieletroniki (simu na Benki) kwa Wahariri na waandishi wa vyombo mbalimbali vya Habari, Jijini Dar es Salaam.troniki (simu na Benki), baada ya kuwasilishwa Bungeni, Dodoma na Mhe. Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.
Baadhi ya Wahariri na waandishi wa Habari wakiwa kwenye Mkutano ulioitishwa na Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam, kutoa ufafanuzi wa tozo za miamala ya kieletroniki (simu na Benki), baada ya kuwasilishwa Bungeni, Dodoma na Mhe. Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)


 Baadhi ya Wahariri na waandishi wa Habari wakimsikiliza Kamishna Msaidizi wa Idara ya Sera Bw. William Mhoja (hayupo picha ni), wakati wa Mkutano ulioitishwa na Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam, kutoa ufafanuzi wa tozo za miamala ya kieletroniki (simu na Benki), baada ya kuwasilishwa Bungeni, Dodoma na Mhe. Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)

Na Scola Malinga, WFM, Dar es Salaam.                                                                                                       

Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uchambuzi wa Sera wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. William Mhoja, amesema Serikali haina malengo ya kutoza wananchi kodi au tozo kwa ajili ya kuwapa mzigo, bali inalenga kuwahusisha watanzania wote kwa umoja katika juhudi za kujikwamua kimaendeleo.

Alisema kuwa Serikali inaendelea kupokea ushauri kuhusu tozo mbalimbali zinazotozwa na serikali na kwamba marekebisho mbalimbali yanaendelea kufanyika.

Bw. Mhoja aliyasema hayo Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wahariri pamoja na waandishi wa vyombo vya habari kuhusu hatua ya serikali ya kufuta baadhi ya tozo za miamala ya kieletroniki, ikiwemo huduma za kuhamisha fedha kutoka benki kwenda mitandao ya simu na kuhamisha fedha ndani ya benki moja na tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki moja kwenda nyingine, akieleza kuwa mambo hayo yamefanyiwa kazi.

Alisema, serikali ni sikivu na hatua aliyochukua Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt Mwingulu Nchemba ya kufuta tozo tatu za miamala ya kielektroniki ni ya kupunguza gharama kwa wananchi na kuendela kupokea maoni mbalimbali na ushauri kwa wadau.

“Serikali imechuka hatua baada ya kupokea ushauri na maoni ya wadau wakiwemo mabenki, wananchi na wadau wengine, na hii imepelekea kufutwa kwa tozo na kupunguza gharama ya miamala kwa asilimia 10 hadi 50 kuligana na kundi la muamala husika” alisema Mhoja

Alisema utekelezaji wa uamuzi huo utaanza Oktoba Mosi mwaka huu na kuwataka wananchi kuendelea kulipa kodi ili serikali ikusanye mapato yake na kuyatumia kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi.

Akizungumza kuhusu mikakati ya serikali katika kupanua wigo wa walipa kodi nchini, Mhoja alisema kampeni ya dai risiti na toa risii ni moja ya mkakati wa serikali kuhakikisha kila malipo yanapofanywa kodi ya serikali inalipwa.

Aidha, Bw. Mhoja alisema kuwa hatua nyingine ya kuongeza wigo wa walipakodi ambao serikali inaendelea kuchukua na kuhimiza ni kuhakikisha wananchi wote wanaostahili kulipa kodi wanalipa na hiyo ni pamoja na kuwaigiza kwenye mfumo wa walipakodi wapya.

Alifafanua kuwa serikali imesamehe tozo ya miamala ya kwenye utoaji wa fedha taslimu kupitia wakala wa benki, na mashine za kutolea fedha (ATM) kwa miamala yenye thamani isiyozidi Sh 30,000.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.