Habari za Punde

Maandalizi ya Uzinduzi wa Matokeo ya SENSA.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Bw. Kaspar Mmuya  akizungumza wakati wa kikao cha Kamati Tendaji iliyohusisha Makatibu wa Wakuu kwaajili ya maandalizi ya Uzinduzi wa Matokeo ya Kwanza ya Sensa ya Watu na Makazi  utakaofanyika Oktoba 31,2022 Katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

NA. MWANDISHI WETU - DODOMA

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Bw. Kaspar Mmuya  Oktoba 25, 2022 ameongoza Kikao cha Kamati Tendaji inayohusisha Makatibu Wakuu Kwaajili ya  Maandalizi ya Uzinduzi Wa Matokeo Ya Kwanza ya Sensa ya Watu na Makazi  Utakaofanyika Oktoba 31,2022 Katika Uwanja Wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Katika uzinduzi huo  mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Takwimu Bi. Ruth Minja akitoa taarifa ya  mwongozo wa uzinduzi huo utakavyofanyika wakati wa kikao hicho.
Baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo wakifuatilia kikao hicho.
Baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo wakifuatilia kikao hicho.

Mratibu wa Sensa Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Adela Mpina akitolea ufafanuzi baadhi ya taarifa zilizowasilishwa za maandalizi ya Uzinduzi huo.

Baadhi ya Makatibu wa Wakuu wakifuatilia hoja za kikao hicho kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt. Francis Michael, katikati ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban na Kulia ni   Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba, na Maendeleo ya Makazi Dkt. Allan Kijazi.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.