Habari za Punde

DKT. NCHEMBA ATETA NA WAWEKEZAJI SEKTA YA BIMA KUTOKA INDIA

Kamisha wa Idara ya Fedha za Nje Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Rished Bade, (wa pili kushoto), akifafanua jambo wakati Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa wawekezaji katika sekta ya bima kutoka India wakiongozwa na Balozi wa India nchini Tanzania Mhe. Binaya S. Pradhan, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.

Balozi wa India nchini Tanzania Mhe. Binaya S. Pradhan (katikati), akiwa na ujumbe wa wawekezaji walioonesha nia ya kuwekeza katika sekta ya bima nchini, wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani) walipokutana na kufanya mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiwa na Balozi wa India nchini Tanzania Mhe. Binaya S. Pradhan, baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiteta jambo na Balozi wa India nchini Tanzania Mhe. Binaya S. Pradhan, aliyeongoza ujumbe wa wawekezaji katika sekta ya bima kutoka nchini mwake walioonesha nia ya kuwekeza katika Sekta hiyo nchi, walipokutana na kufanya mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb)(wa tano kulia), akiwa katika picha ya Pamoja na ujumbe wa wawekezaji wa sekta ya bima kutoka nchini India wakiongozwa na Balozi wa India nchini Tanzania Mhe. Binaya S. Pradhan (wa tatu kulia), walipokutana na kufanya mazungumzo Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha na MIpango, Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipngo-DSM)
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.