Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary
Masanja (Mb) amewataka wananchi waliovamia Msitu wa Kuni na kuanzisha shughuli
za ujenzi wa nyumba, kuacha mara moja na kuondoka katika eneo hilo la hifadhi .
Ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na
wananchi katika Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro.
“Sasa tunachowaomba kwanza kusimamisha ujenzi
kwenye eneo la msitu ,pili tutaangalia wale ambao wamejimilikisha maeneo
makubwa lazima tuyagawe kwa sababu wote
ni wavamizi” amesisitiza Mhe. Masanja.
Amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa huruma yake aliruhusu eneo la msitu
limegwe jumla ya hekta 2000 ambazo zitagawiwa kwa wananchi lakini wananchi
wameendelea kulivamia eneo la msitu.
“Mwaka jana tukaelekeza wananchi wapangwe
kwenye hekta elfu 2000 na hiyo ni huruma ya Mheshimiwa Rais Samia kwanza naomba
tumpongeze mama yetu ana huruma kwa
sababu ilikuwa muondolewe lakini akasema hapana hawa ni wananchi wangu
wapangwe” Mhe. Masanja amefafanua.
Ameweka bayana kuwa wananchi waliomo kwenye hekta
elfu 2000 zilzizogawiwa wako kihalali na watapimiwa ardhi na kupewa hati zao lakini waliovamia wanapaswa
kuondoka katika eneo hilo.
Katika hatua nyingine , Naibu Waziri Masanja
amewaasa wananchi wa Kijiji cha Ngombo Wilayani Malinyi, kuhifadhi mazingira na
kuacha tabia ya kukata miti hovyo kwa faida ya kizazi cha sasa na cha baadae.
No comments:
Post a Comment