Baadhi ya Maafisa wa Habari na Mawasiliano kutoka Wizara na taasisi za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakimsikiliza Mkurugenzi (hayupo pichani) walioshiriki katika kikao cha Maafisa wa habari na Mawasiliyano kilichofanyika katika ukumbi wa Radio Rahaleo Zanzibar.
Picha na Miza Othman-Maelezo Zanzibar.
Na Ali Issa Maelezo 23/12/2022
Maafisa wa Habari na Mawasiliano nchini wametakiwa kutumia vyombo vya habari kwa kutoa taarifa za utendaji wa kazi katika Ofisi zao kwa lengo la kuihabarisha jamii.
hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Habari Maelezo Hassan Khatib Hassan wakati akizungumza na Maafisa Habari na Mawasiliano wa Wizara tofauti katika ukumbi wa Sanaa, Rahaleo.
Amesema inapotolewa habari ya Wizara au Taasisi katika vyombo vya habari ,jamii itaweza kufahamu kinachofanyika katika Serikali yao na kusaidia kuonyesha ufanisi wa kazi
Amesema jambo hilo hupelekea kuonesha dhamira ya kweli kwani kunamasuala mengi ya kimaendeleo yametekelezwa.
“Mengi mazuri yapo yaliofanywa na Serikali hivyo ni vyema kuyaonesha kwa kuandika ,” alisema Mkurugenzi.
Aidha alifahamisha kuwa kuwepo na ushirikiano na waandishi wa habari pale ambapo wanapohitaji taarifa za Wizara au Taasisi wazipate bila ya usumbufu.
Hata hivyo aliwataka kuwa pamoja na Idara ya Habari Maelezo kwa kutuma taarifa zao pale ambapo kuna tukio la utekelezaji.
Nae Afisa Habari Muandamizi Salum Abdalla amesema Maafisa Habari ni watu muhimu katika kusimamia kazi za wizara au taasisi zao ikiwa ni moja ya majukumu yao .
Hatahivyo aliwaeleza Maafisa hao kuwa karibu na Viongozi wa Taasisi zao ili kupata taarifa zinazotokea na kufahamu yaliopo.
Nae Afisa habari kutoka Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Kassim Abdi aliwafahamisha Maafisa hao kuandaa mpango kazi na kuuwasilisha katika vikao vya viongozi wao ili kupunguza changamoto zinazojitokeza katIka Wizara au Taasisi zao .
No comments:
Post a Comment