Habari za Punde

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Philip Mpango Akishiriki Ibada ya Krismas Dodoma

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.Philip Mpango pamoja na mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakishiriki Ibada ya Misa takatifu ya Sikukuu ya Krismasi iliofanyika katika Parokia ya Kristo mfalme iliopo Veyula mkoani Dodoma leo tarehe 25 Desemba 2022.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.Philip Mpango pamoja na mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakishiriki Ibada ya Misa takatifu ya Sikukuu ya Krismasi iliofanyika katika Parokia ya Kristo mfalme iliopo Veyula mkoani Dodoma leo tarehe 25 Desemba 2022.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.Philip Mpango ametoa wito kwa watanzania kuongeza jitihada katika kuimarisha ulinzi wa watoto ili kuwaepusha na vitendo vya ukatili vinavyowakumba hivi sasa.

Makamu wa Rais amesema hayo mara baada ya kushiriki Ibada ya Misa Takatifu ya Sikukuu ya Krismasi katika Parokia ya Kristo mfalme iliopo Veyula mkoani Dodoma. Ametoa wito kwa watanzania kuomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu kwa matendo ya kikatili kwa Watoto na kuacha dhuluma dhidi yao. Aidha amewasihi waumini na watanzania kwa ujumla kutimiza mahitaji ya watoto katika kuwatunza ikiwemo kuhakikisha wanapata elimu.

Halikadhalika Makamu wa Rais ametoa wito kwa watanzania kutumia fursa ya uwepo wa mvua zilizoanza kunyeesha hapa nchini katika kuzalisha mazao pamoja na kupanda miti ili kuhifadhi mazingira. Amesema ni muhimu suala la upandaji miti kuanza katika ngazi ya familia kwa kupanda miti mitatu kila familia na hivyo kupendezesha nchi na kulinda mazingira.

Katika ibada hiyo, Makamu wa Rais ameambatana na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango na ibada imeongozwa na Paroko wa Parokia ya Kristo Mfalme iliyopo Veyula Dodoma Padre Saimon Katembo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.