Habari za Punde

SMZ itaendelea kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020 – 2025 kwa Vitendo




 Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020 – 2025 kwa Vitendo ili Wananchi wa Zanzibar wapate kufaidika na Miradi mingi ya Serikali.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameyasema hayo wakati akiwasilisha Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020 – 2025 kwa kipindi cha Miaka Miwili aliyoitoa  katika Mkutano Mkuu wa Kumi wa Chama cha Mapinduzi Taifa uliofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Dodoma.

Ameeleza kuwa Uchumi wa Zanzibar umekuwa kwa kasi wa wastani wa Asilimia 5.1 kwa Pato la Taifa Mwaka 2021 ikilinganishwa na Asilimia 1.3 Mwaka 2020 hatua ambayo inatoa matumaini ya kuwaletea Maendeleo Wananchi wake.

Amesema kuongezeka kwa Pato la Taifa kunaisadia Serikali kuweza kupanga Mipango endelevu ya kuwaletea Maendeleo Wananchi wake kwa Asilimia kubwa.

Mhe. Hemed ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ameeleza kuwa Serikali imeweza kutekeleza Miradi mbali mbali ya Maendeleo ambayo inawagusa moja kwa moja Wananchi wake ikiwemo ujenzi wa Hospitali katika Wilaya Kumi za Zanzibar pamoja na Hospitali moja ya Mkoa inayojengwa Lumumba Mkoa wa Mjini Magharibi .

Aidha ameeleza kuwa Serikali imeboresha Miundombinu ya Elimu kwa   kujenga Skuli 42 zikiwemo Skuli 28 za Maandalizi, Skuli 10 za Msingi na Skuli 4 za Sekondari hatua ambayo inasaidia kupunguza uhaba wa majengo. 

Akigusia Huduma ya upatikanaji wa Maji safi na salama Mhe. Hemed ameeleza kuwa Serikali imefanikiwa kusambaza Huduma hiyo katika Shehia 342 kati ya Shehia 388 sambamba na Mradi wa Ujenzi wa Matangi makubwa Mradi ambao kukamilika kwake kutamaliza changamoto ya upatikanaji wa maji katika Shehia zote za Unguja na Pemba.

Sambamba na hayo Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya CCM Taifa amewashukuru Wananchi wa Zanzibar kwa mashirikiano wanayaoendelea kuipatia Serikali na Chama Cha Mapinduzi katika kufikia malengo waliojiwekea.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Chumbuni ambae pia ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Mhe. Ussi Salum Pondeza ameeleza kuwa juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ni za kupongezwa na kueleza kuwa utekelezaji huo umeweza kuwafikia wananchi wote wa Zanzibar.  

Nae Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Hayam Mustafa Yakout amepongeza juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Awamu ya Nane inayoongozwa na Dkt. Hussein Ali Mwinyi ikiwemo ujenzi wa Hospitali ambazo zitakuwa na huduma muhimu hasa huduma za kina mama

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.