Habari za Punde

Waziri Mhe.Simbachawene, Amepokea apokea madawati

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akipokea madawati  ya  Kisima Umoja Vijana.

Na mwandishi wetu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene amepongeza vijana waliojiunga katika Kikundi cha Kisima umoja Vijana kwa moyo wao wa uzalendo wa kuchangia  madawati katika shule ya Msingi Kisima.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu (Mb) Mhe. George Simbachawene  katika ziara yake ya kutembelea na Kuzungumza na wananchi katika Jimbo lake la uchaguzi  Kibakwe Halmashauri ya Mpwapwa.

“Vijana  wameweza kuchangia madawati 14 yenye thamani karibu ya million moja, ni jambo kubwa na vijana wengine igeni mfano wa vijana hawa.”

Wamekumbuka Nyumbani wameona wadogo zao wakae mahali pazuri kwa kuamua kutengeneza madawati, na umoja wao ni wa watu ambao hawana kitu lakini ni umoja ambao unadhamira.

“Jambo la msingi katika maisha ni kuwa na dhamira na  jambo lako, kwa sababu Mungu anabariki mipango, Mungu anabariki dhamira,” alisema Waziri.

Kwa niaba ya viongozi serikalini na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi naomba niwashukuru sana kwa tendo hili linaloonesha umoja ni nguvu.

Akisoma taarifa ya  Kikundi cha Kisima Umoja Vijana, mbele ya Waziri  Bwn.  Kepher  Mdachi amesema malengo yao ni kuendelea kusaidia jamii yetu na ambazo ziko ndani ya uwezo wa kikundi hicho.

“Kutoa hamasa kwa wanafunzi ili kuongeza ufaulu, kutoa elimu kwa jamii kwa kuwafikia wazazi na walezi ili kuwahamasisha umuhimu wa elimu kwa vijana wao.”

Aidha kikundi hicho kimelenga kujenga taasisi imara itakayolenga kusaidia jamii na kufanya jambo la kijamii kila mwisho wa mwaka ikiwa pamoja na kusaidia sekta ya afya kwa kuchangia vifaa tiba vyenye uhitaji wa haraka.

“Madawati haya yamepatikana kutokana na utaratibu wa kutoa ada kwa kila mmoja kuanzia shilingi 2000 kadiri anavyojaliwa, na hufanywa kwa hiari.  Tumezidi kuwa wamoja pale tunaposikia changamoto za kijamii ikiwa ni pamoja na kusaidiana sisi wenyewe kama mmoja wanakikundi amepata shida,” alisema Mdachi. 


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akimkabididhi Mwenyekiti wa kijiji cha Kisima madawati.

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na vijana wa kikundi cha Kisima Umoja Vijana.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.