Habari za Punde

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akutana na Kuzungumza na Waziri Mkuu Mstaafu wa Ethiopia Mhe. Hailemariam Desalegn, Dakar Senegal

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu wa Ethiopia Mhe. Hailemariam Desalegn aliyeambatana na ujumbe wake Dakar, Senegal tarehe 26 Januari,2023. Pamoja na mambo mengine, katika kikao hicho wamezungumzia jinsi ambavyo Tanzania imejiandaa kuwa mwenyeji wa Mkutano mkubwa wa Kilimo utakaohusisha, viongozi, watu mashuhuri na Wadau wapya 3,000. Waziri Mkuu Mstaafu wa Ethiopia Mhe. Hailemariam Desalegn  ni Mwenyekiti wa Africa's Food Systems Forum (AGRF)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu wa Ethiopia Mhe. Hailemariam Desalegn pamoja na ujumbe wake mara baada ya mazungumzo Dakar nchini Senegal tarehe 26 Januari, 2023. wengine katika Picha ni Waziri wa Kilimo Hussein Bashe pamoja na Viongozi wengine kutoka Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na  Waziri Mkuu Mstaafu wa Ethiopia Mhe. Hailemariam Desalegn ambaye pia ni Mwenyekiti wa Africa's Food Systems Forum (AGRF) mara baada ya mazungumzo yao  Dakar, Senegal tarehe 26 Januari, 2023. 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Marais wa nchi mbalimbali za Afrika wakati akizungumza kwenye Mkutano wa Kilimo na Chakula kwa Bara la Afrika  uliofanyika Dakar nchini Senegal.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.