Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Reginant kivinge akiongea wakati wa kupitisha bajeti hiyo mbele ya wananchi,wadau na madiwani wa Halmashauri ya Mji Mafinga
Baadhi ya madiwani, wataalam na baadhi ya wananchi wakifuatilia namna ya Baraza la madiwani lilipokuwa linaendelea
Na Fredy Mgunda, Iringa.
HALMASHAURI ya Mafinga Mji imepitisha bajeti ya shilingi bilioni 29.32 kwa mwaka wa fedha wa 2023/2024 kwa ajili ya maendeleo ya wananchi pamoja na matumizi ya ofisi.
Akizungumza katika kikao cha baraza la Madiwani,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Reginant kivinge alisema kuwa bajeti hiyo imejikitaka katika mishahara na matumizi mengine ya utendaji wa Ofisi ya Halmashauri hiyo.
Kivinge alisema kuwa katika mwaka wa fedha wa 2023/2024 Halmashauri ya Mji Mafinga inatarajia kupokea kiasi cha shilingi bilioni 6.35 kutoka serikali kuu, shilingi bilioni 1.81ni mapato ya ndani na shilingi bilioni 3.56 za mapato ya nje.
Alisema kuwa rasimu bajeti hiyo imejielekeza pia katika kuboresha mtandao wa barabara za mjini na vijijini, ngazi ya kata kwa kufanya matengenezo, utekelezaji wa makundi maalum kwa kuelekeza asilimia 10 ya makusanyi ya mapato ya ndani.
Kivinge alisema kuwa fedha hizo zitatumika katika kukamilisha miundombini ya kutolea huduma kwa jamii katika sekta ya afya, elimu na utawala.
Alisema kuwa Halmashauri iataendelea kushirikiana na jamii,wadau, serikali kuu,ofisi ya mkuu wa mkoa na wilaya ya Mufindi pamoja na chama cha mapinduzi ngazi zote katika kuhakikisha wanachangia mpango wa bajeti ya Halmashauri hiyo.
Kivinge alisema kuwa anampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka fedha nyingi za miradi ya kimaendeleo katika Halmashauri ya Mji Mafinga hatua inayochochea maendeleo na utatuzi wa changamoto ya huduma mbalimbali ikiwemo Huduma za afya, Elimu na miundombinu ya kiuchumi.
Lakini pia chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi kimelitaka baraza la madiwani Halmashauri Mafinga Mji kuhakikisha linashughulikia kwa wakati kero za wananchi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji kwa vitendo Ilani ya CCM na kuwaonya viongozi wanaowakumbuka wananchi pindi uchaguzi unapokaribia
Akizungumza kwenye baraza la madiwani la Halmashauri ya Mji Mafinga ,mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Mufindi George Kavenuke alisema kuwa suala la barabara,maji,afya,elimu na masoko imekuwa changamoto kubwa kubwa kwa wananchi hivyo viongozi wa serikali ya Halmashauri ya Mafinga Mji wanatatua changamoto zote hizo ili chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Mufindi kuendelea kushika dola kama ambavyo ilivyo hivi Sasa.
No comments:
Post a Comment