Habari za Punde

Dr Dimwa asisitiza mshikamano kati ya viongozi na wanachama

KADA wa Chama Cha Mapinduzi Ibrahim Raza(upande wa kulia), akimkabidhi kompyuta Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohammed Said Mohammed ‘Dimwa’ (upande wa kushoto), makabidhiano hayo yamefanyika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Unguja.

NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk. Mohammed Said Mohammed 'Dimwa',amesema umoja na ushirikiano baina ya wanachama,viongozi na watendaji utasaidia kuongeza ufanisi wa kiutendaji ndani ya Chama.

Hayo ameyasema mara ofisini kwake Kisiwandui Mjini Unguja mara baada ya kupokea vifaa vya kompyuta kutoka kwa kada wa CCM Mbunge mstaafu wa Jimbo la Kiembesamaki Ibrahim Raza.

Alisema Chama Cha Mapinduzi kinaendeshwa kwa misingi ya kujitolea hivyo kila mwanachama ana haki na wajibu wa kutoa mchango wake wa hiari kwa nia ya kuimarisha chama.

Alieleza kuwa misingi hiyo imejengwa na waasisi wa CCM toka enzi za Chama Cha Afro-Shiraz Party(ASP),waliotoa michango mbalimbali kwa lengo la kujiimarisha kisiasa,kiuchumi na kijamii.

“Komputa hii itasaidia katika shughuli zetu za kiutendaji na tunakuahidi itatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.

Tumeupokea msaada na tunaamini kuwa Ibrahim Raza ni kada mwaminifu wa CCM na kutupa msaada huu ni kwa mapenzi yake tu ya kuisaidia ofisi hivyo tunamshukuru sana”,alisema Dkt.Dimwa.

Alisema, kukiwa na makada kama hao na wakashirikiana kwa pamoja ni jambo zuri lakini vile vile chama kitawatumia kila mtu kwa nafasi yake na kila mtu kwa uwezo wake.

Kwa upande wake Kada huyo Ibrahim Raza, alisema kompyuta hiyo itakuwa ni chachu ya kuimarisha utendaji wa shughuli za Chama kwa wakati.

Raza ambaye ni mbunge wa zamani wa jimbo la Kiembesamaki, alimuhakikishia Naibu Katibu Mkuu huyo kuwa, yupo tayari kufanya kazi na yeye na kwamba majukumu yoyote atakayopangiwa na Chama cha Mapinduzi.

Pamoja na hayo alisema ataendelea kuwa muumini wa kushiriki katika mikakati ya kuandaa mazingira ya ushindi wa CCM katika uchaguzi mkuu wa dola mwaka 2025.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.